Michezo mwishoni mwa wiki | Michezo | DW | 28.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo mwishoni mwa wiki

Mashindano ya ubingwa wa mbio za nyika Scotland.

Kesho macho ya mashabiki wa riadha yanakodolewa Edinburgh,Scotland ambako majogoo wa Ethiopia wakiongozwa na Kenenisa Bekele wanaumana na wale wa Kenya na Ertirea kunyan'ganyia taji la ubingwa wa dunia wa mbio za nyika-world cross-country chamipionship.

Bekele anaania taji lake la 6 na nani atamzuwia ?

Ronaldinho,siku zake na FC Barcelona zimemalizika -ataelekea wapi msimu ujao ?

Bayern Munich-viongozi wa Bundesliga-ligi ya Ujerumani, wana miadi leo na jirani zao Nüremberg na wanadai hawana shaka watazidi kutanua mwanya wao kileleni kwa pointi 3 zaidi kutoka Nüremberg.

►◄

Ingawa Kenenisa Bekele wa ethiopia anamtazamia bingwa wa mwaka jana huko Mombasa,Kenya, mueritrea Zersenay Tadese kumpa changamoto , ni wakenya ambao wamejiwinda kumzima asitoroke na taji lake la 6 la ubingwa huko Scotland.

Zaidi ya wanariadha 500 kutoka nchi 70 mbali mbali wake kwa waume wataania ubingwa huo wa mbio za nyika za km 12 kwa wanaume na 8 kw awanawake .Pia kuna mashindano ya chipukizi tangu ya wasichana hata wavulana.WEashindi watavuna kitita cha jumla ya dala 228,000.

Bekele ndie bingwa mkubwa kabisa ulimwenguni wa mbio hizi za crosscountry akiwa ametia mfukoni mataji 11 na kesho anasaka taji lake la 6 la ubingwa wa mashindano haya.Mwaka jana, mambo yalimchachia njiani na akabidi kusalim amri huko Mombasa, kwa mueritrea Tadese.

Bekele aliumwa na tumbo njiani na Mueritrea hakuamini bahati yake.

Wakenya ambao mazowezi yao yalipatwa na mkosi nyumbani kutokana na machafuko ya uchaguzi uliopita, wanadai hatahivyo, wamejiandaa vya kutosha kukabili vishindo na hata hali ya hewa ya Edinburgh kama vile mwanamichezo wetu Eric Ponda alivyotuarifu kwa ufupi kutoka Keny

Wakenya wanaotazamiwa kutamba ni pamoja na Gideon Ngatuny.

Mbali na wakenya changamoto pia yaweza kutoka kwa mganda Moses Kipsiro.Nje ya Afrika, macho yatakodolewa kesho kwa Muastralia Craig Mottram.Upande wa wasichana Muethiopia Tirunesh Dibaba atajaribu kutamba katika mbio za nyika .Katika medani ya dimba ,mashabiki wa Ujerumani wa bundesliga, wanaona hakuna timu itayoweza msimu huu kuzima vishindo vya Bayern Munich.Majaribio ya Bremen,Hamburg na hata Leverkusen yote yameshindwa na jioni hii Nüremberg,haitazamiwi kufua dafu licha ya kuwa inacheza nyumbani.

Bayer Leverkusen iliolazwa kwa mabao 2:1 na Munich jumamosi iliopita ina miadi leo na Frankfurt wakati Hamburg inakumbana na Armenia Bielefeld.Schalke inacheza na Karsruhe.

Stadi wa B.munich -zamanib FC Cologne, Lukas Podolski anafikiria kuiachamkono Munich msimu ujao kwani amechoka kuwa mchezaji wa akiba tu.Amesema atafikiria upya mustakbala wake wa dimba baada ya msimu huu.

Endapo klabu yake ya zamani FC Cologne, ikipanda daraja ya kwanza msimu ujao itakua ya kwanza kumtapia Podolski.

Mwengine asieridhika na klabu yake ya sasa ni stadi wa Brazil-Ronaldinho anaetazamiwa kuiaga FC Barcelona katika La Liga.Enzi ya Ronaldinho huko Spian imemalizika-magazeti ya spain yalinadi kati ya wiki hii na hata kocha wake was zamani Carles Rexach.

Ronaldinho amekuwa akikalia benchi tu karibuni na yaonesha amekorofishana na uongozi wa Barcelona.

Barcelona leo inacheza na Real Betis iwapo Ronaldinho atakuwa uwanjani au la ,tusubiri kuona.Atletico madriod inacheza na Villareal wakati Real madrid ina kumbana na Sevilla.

Ama katika zahama za Premier League huko Uingereza,Liverpool itacheza kesho jumapili bila ya Javier Mascherano kati yake na Everton mechi muhimu ya,kuania nafasi ya 4 ya ngazi ya premier league.

Viongozi wa Ligi-Manchester united ina miadi na Aston Villa ,pengine bila ya Louis Saha alieumia.Chelsea iliopo nafasi ya pili itakua uwanjani kesho kama Liverpool ikicheza na Middlesbrough.