Michezo mwishoni mwa wiki | Michezo | DW | 21.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Michezo mwishoni mwa wiki

Kinyan'ganyiro cha kombe la klabu bingwa na la shirikisho barani afrika kinarudi uwanjani.

default

Bayer Leverkusen na B.Munich

Duru ya pili ya kombe la klabu bingwa barani afrika-champions-league na ile ya kombe la shirikisho la dimba la Afrika-Confederations cup -inarudi uwanjani huku macho ya mashabiki yakiukodolea mpambano kati ya mabingwa Etoile du sahel na AS Douanes ya Senegal.Enyimba ya Nigeria inawakaribisha simba wa Tanzania. Al Ahly ya Misri-makamo-bingwa imepata bure ya kuingia duru ijayo baada ya mahasimu wao Al-Tahrir ya Eritrea kujitoa.

Katika Bundesliga-ligi ya Ujerumani viongozi wa ligi-Bayern Munich wana miadi leo na Bayer Leverkusen iliochukua nafasi ya Werder Bremen kuifukuzia munich kileleni.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza,tottenham Hotspur inaklutana na Portsmouth wakati Bolton Wanderers inacheza na Manchester City.

Katika kinyan'ganyiro cha kombe la klabu bingwa barani Afrika, Zamalek ya Misri ambayo kama wenzake Al Ahly wametwaa kombe hilo mara 5 kila moja, wanawakaribisha nyumbani Cairo Africa Sports ya Ivory Coast.Mpambano huu ni marudio ya finali ya kombe hili ya mwaka 1986 ambayo ilimalizika kwa ushindi wa Zamalek kupitia changamoto za mikwaju ya penalty huko Cairo.

Zahama hii inafufua uhasama kati ya Tembo wa Ivory Coast na mafiraouni wa dimba wa Misri uliopata kasi kuanzia finali ya kombe la mataifa 1986 mjini Cairo.

hata finali ya kombe lililopita la Afrika mjini Accra Ghana,Tembo wa ivory Coast walikanyagwa kwa mabao 4-1 na Misri.

ASEC ABIDJAN pia ya ivory Coast mara hii iliteleza na mapema mwaka jana ,lakini msimu huu Asec imepania na yatazamiwa mwishoni mwa wiki hii kutamba nyumbani Abidjan mbele ya AS Kaloum ya guinea.

Enyimba ya Nigeria ina miadi leo na simba ya Tanzania na simba walituma na mapema salamu zao kwa Enyimba kwamba wamekusudia kunguruma huko Nigeria:

lakini licha ya salamu hizo za simba ,wasisahau kwamba Enyimba ni mojawapo ya klabu 3 tu za Afrika zilizoshinda na kulitetea taji lao na Enyimba haitaki mwaka huu kurudia madhambi ya mwaka uliopita ilipoaga kombe hili na mapema.

Dynamo ya Zimbabwe inakumbana na Costa do Sol ya msumbiji katika zahama ya timu 2 za kanda ya Cosafa.

Mabingwa Etoile du sahel ya tunisia hawana wasi wasi leo wakicheza nyumbani na chipukizi AS Douanes ya Senegal.

Etoile lakini ina wasi wasi wa kumkosa mshambulizi wao Amine Chermiti aliepachika mabao 8 yaliopelekea etoile hata kutamba mwishoe mbele ya Al Ahly ya Misri na kutoroka na ubingwa.

Ama katika kinyan'ganyiro cha Kombe la shirikisho-Confederations Cup-mabingwa wa kombe hili Sfaxien pia ya Tunisia haitambi sana msimu huu kama uliopita.Sfaxien huenda isimudu vishindo vya watunisia wenzake Esperence iliowafungisha mikataba mastadi kadhaa wa nyumbani.Young Africans ya Tanzania ina miadi huko Libya na Al-Akhdar.

Bundesliga-ligi ya Ujerumani pia inarudi leo na kesho viwanjani: viongozi wa ligi-Bayern Munich wana kibarua kigumu leo licha ya kuwa wanahemkwa nyumbani wakicheza na Bayer Leverkusen.Hamburg ilioparamia ngazi ya Ligi hadi nafasi ya pili nyuma ya munich huenda leo ikakiona cha mtema kuni kutoka majirani zao Wolfsburg ambayo mwihoni mwa wiki iliopita iliichezesha Bremen-klabu nyengine ya kileleni mwa Ligi kindumbwe-ndumbwe na kuitoa kwa bao 1:0.

Mabingwa Stuttgart wamekuwa wakitamba karibuni na wanaelekea kileleni.Leo wana miadi na Hansa Rostock na wakicheza nyumbani hawana shaka pointi 3 zitakuwa kibindoni.Nüremberg wanacheza na Bochum na duisburg inaikaribisha nyumbani Hannover.

Ama Premier League-Ligi ya Uingereza ,leo inaziita uwanjani Tottenham Hotspurs kuumana na Portsmouth wakati Aston Villa inapiamana nguvu na Sunderland.

Blackburn Rovers inacheza leo na Wigan Athletics wakati Bolton Wanderers inachuana na manchester city.

Katika La Liga-Ligi ya Spian,kuna changamoto 2 leo-moja ni kati ya Real malloca na Deportivo la coruna na sevilla inachuana na Atletico Madrid.

Kwenye serie A-Ligi ya Itali -viongozi wa ligi Inter milan wanacheza na Juventus wakati Ac Milan, wanaitembelea Torino.Reggina inapapurana na Napoli wakati Roma wamejiandaa nyumbani kutamba mbele ya Empoli.

kati ya wiki ijayo, ni zamu ya kinyan'ganyiro cha kombe la dunia kuania tiketi za 2010 nchini afrika kusini kwa kanda ya Asia:Thailand ina miadi na Oman wakati Kuweit inacheza na Iran.Uzbekistan ni mwenyeji wa Saudi Arabia.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com