Michezo mwishoni mwa wiki | Michezo | DW | 06.03.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo mwishoni mwa wiki

Mashindano ya ubingwa wa riadha ya dunia yaanza leo huko Sevilla,Spian pamoja na majogoo wa afrika.

Miroslav Klose wavuni

Miroslav Klose wavuni

Michezo ya olimpik ya Beijing ikinyemelea ,wanariadha wake kwa waume miongoni mwao mkongwe Maria Mutola wa Msumbiji wamewasili Valencia ,Spain kwa changamoto za mwishoni mwa wiki hii za ubingwa wa riadha wa dunia ukumbini-world Indoor Athletics Championship wakijinoa kwa Olimpik.

Oliver Kahn aliekua kipa wa Taifa wa Ujerumani analinda lango la Bayern Munich akicheza leo mpambano wa mwisho na klabu yake ya zamani Karlsruhe katika Bundesliga.Baada ya Arsenal London kuwavua taji mabingwa wa Ulaya AC Milan kati ya wiki katika champions League- imeazimia kupanua mwanya wake hadi pointi 4 mradi tu iishinde kesho Wigan Athletics. Huko Ufaransa, lyon licha ya kupigwa kumbo nje ya champions League na Manchester united imepania kuendelea kutamba kesho mbele ya Bordeaux na kutwaa taji lake la 7 la Ligi ya Ufaransa.

Ramadhan Ali anatunfungulia pazia la viwanja vya michezo mwishoni mwa wiki hii:

Macho ya hasa mashabikiwa riadha na michezo ijayo ya olimpik ya kiangazi mjini Beinjing,China Augosti hii lazima yanakodolewa Sevilla,Spain .Miongoni mwa malikia wa mbio wa Afrika huko Spain ni bingwa wa zamani wa olimpik wa mita 800 na wa dunia-Maria Mutola wa Msumbiji, bingwa wa dunia wa mita 5000 muethiopia Meseret Defar na hata wanariadha wake kwa waume kutoka Kenya iliofufuka majuzi tu kutoka machafuko ya kisiasa.

Kwa Maria Mutola,bingwa mkubwa kuliko wote wakike katika mashindano ya ukumbini-indoor,Sevilla, ni medani maalumu akiania medali yake ya 8 ya dhahabu kabla hakustaafu mwishoni mwa msimu huu wa Olimpik baada ya kutamba kwa miaka 15.

Maria Mutola amenukuliwa kusema kabla kuingia uwanjani huko Sevilla kwamba ana shabaha mbili mwaka huu:“Kwanza kutetea taji langu la ubingwa mjini Sevilla na shabaha ya pili ni kunyakua medali ya dhahabu mjini Beijing.“ Lakini akiwa na umri wa miaka 35,Mutola anajua haitakua rahisi kutimiza shabaha hizo 2,kwani Kenya ilitoa bingwa wa dunia katika michezo ya mwaka jana ya ubingwa wa riadha wa dunia nae amepania pia kutawazwa bingwa wa Olimpik huko Beijing.

Muethiopia Meseret Defar ni mmoja kati ya mabingwa 4 wa dunia wa nje na ukumbini mjini Valencia mwishoni mwa wiki hii na yeye ndie bingwa wa Olimpik na dunia wa masafa ya mita 5000.Anatazamiwa sana kumuigiza mromania gabriela Szabo kushinda taji lake la 3 mfululizo la mita 3000.

Upande wa wanaume,mkenya Wilfred Bungei hataweza kutetea taji lake la mita 800 kwavile ameumia lakini mwenzake Daniel Kipchichir Komen ndie aliopo usoni katika mita 1.500 akikimbia muda bora duniani mwaka huu wa olimpik.

Katika viwanja vya dimba,Ligi mashuhuri za Ulaya zinarudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii baada ya changamoto za kati ya wiki za champions League- kombe la klabu bingwa barani ulaya na la UEFA-shirikisho la dimba la Ulaya:

Schalke ya Ujerumani iliopatwa na mkosi mkubwa wa kupokonywa pointi 3 nyumbani jumamosi iliopita na viongozi wa Ligi-Bayern Munich walitamba katika kombe la klabu bingwa la Ulaya walipoitoa Porto ya ureno katika changamoto ya kusisimua ajabu ya mikwaju ya penalty.Leo basi imepania kufuta madhambi ya kushindwa mara 3 mfululizo katika Bundesliga na kutupwa nafasi ya 6 ya ngazi ya Ligi.Mwishoni mwa wiki hii Schalke ina miadi na Bielefeld iliopo nafasi ya 4 kutoka mkiani.

B.Munich inampa nafasi langoni kipa wake Oliver Kahn nafasi ya mwisho kucheza na klabu yake ya zamani Karlsruhe.Munich inaelewa Karlsruhe, si kuteremka mlima. Bremen iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi na pointi 4 nyuma ya Bayern wanawatembelea leo mabingwa stuttgart wakati hamburg iliopo nafasi ya 3 watatimuana na Nüremberg hapo kesho huko kusini mwa Ujerumani.

Manchester United na Chelsea zikijishughulisha na Kombe la FA mwishoni mwa wiki hii,viongozi wa Ligi Arsenal wana nafasi ya kupanua mwanya wao uliopunguzwa hadi pointi 1 tu na kuugeza pointi 4.Mradi tu watambe kesho mbele ya Wigan Athletics.Na Arsenal ina kila sababu ya kutamba kwani kati ya wiki ni wao waliowavua taji la Ulaya mabingwa AC milan tena uwanjani mwao San Rio,Itali.

Olympique Lyon ya Ufaransa inaamini kwamba machozi yake iliotoa ilipolazwa majuzi na Manchester united katika champions League, yatatosha kuitia shime nyumbani kutamba kesho mbele ya girondins Bordeaux na kuvaa taji lao la 7 la ubingwa.Bordeaux iko nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi.

Katika La Liga-ligi ya Spian, mashabiki wa Real Madrid –mabingwa mara 9 wa Ulaya wanahofia msiba uliowakumba kwa kutolewa na mapema nje ya kombe hilo la Ulaya usije ukawapata pia katika la Liga.juzi jumatano Real Madrid ilipigwa kumbo tena nyumbani na AS Roma ya Itali ilipochapwa mabao 2-1 na kuaga kombe hilo.Real inaongoza hatahivyo Ligi ya Spain kwa pointi 5 mble ya Barcelona na leo ina miadi na Espanyol iliopo nafasi ya 5 lakini Real inabidi kucheza bila ya jogoo lao van Niestelrooy.

 • Tarehe 06.03.2008
 • Mwandishi Ramadhan aliMichezo ya olimpik ya Beijing ikinyeme
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DJjb
 • Tarehe 06.03.2008
 • Mwandishi Ramadhan aliMichezo ya olimpik ya Beijing ikinyeme
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DJjb