michezo mwishoni mwa wiki | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 11.01.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

michezo mwishoni mwa wiki

Kombe la 26 laafrika laanza jumapili Januari 20 mjini Accra.Ghana wenyeji wanafungua dimba na Guinea.

Mwishoni mwa wiki ijayo firimbi italia kuanzisha mjini Accra Kombe la 26 la Afrika la Mataifa na timu kadhaa za taifa zimo kutangaza vikosi vyao vya wachezaji 23 wa mwisho ,baadhi ya ligi mashuhuri barani Ulaya ziko uwanjani mwishoni mwa wiki hii ingawa bila ya baadhi ya mastadi wao wa Afrika-kama vile Michael Essien wa Ghana,Didier Drogba wa Ivory Coast na Samuel Eto’o wa Barcelona.

Mabingwa mara kadhaa waUjerumani –Bayern Munich wametangaza jana kuwa kocha mpya msimu ujao ni Jürgen klinsmann alieongoza Ujerumani katika finali za kombe la dunia lililopita 2006 na kumaliza nafasi ya 3 nyuma ya Itali na Ufaransa.

Manchester united imetangaza kuvuna kitita kikubwa kilicho rekodi cha dala milioni 478.3 katika msimu wa 2006/07 na hivyo wathibitisha hadbi yao kuwa klabu tajiri kabisa duniani.

Manchester united ya Uingereza kabla kuingia uwanjani leo na New Castle United ilitangaza kwamba imevuna kitita cha pauni sterling mil.478.3 na hivyo wamethibitisha hadhi yao kuwa klabu tajiri kabisa ya dimba ulimwenguni.hii inatokana na kuupanua uwanja wake wa old Trafford kuhudumia hadi mashabiki 76.000.Manchester ikatangaza pia kuwa majira ya kianza yajayo itafunga safari ya afrika Kusini kwa maandalio ya msimu mpya. Isitoshe,manchester united iliweka wazio wazi na tena hadharani kwamba jogoo lao la ureno-Cristiano Ronaldo haliuzwi tena kwa bei yoyote ile.Ronaldo ameshapachika mabao 19 kwa manchester msimu huu na mreno huyo anapigiwa upatu kuwa mmoja kati ya mastadi wakubwa wa dimba duniani wakati huu.

Ligi ya Ujerumani-bundesliga ingali bado mapumzikoni tangu X-masi na mwaka mpya.Hatahivyo, imeendelea kugonga vichwa vya habari.Kwanza Bayern munich –viongozi wa ligi imemtangaza kocha wake mpya msimu ujao.Kuanzia Julai mosi,mwaka huu, Jürgen klinsmann alieiiongoza Ujerumani hadi nafasi ya 3 ya kombe la dunia nyuma ya mabingwa Itali na makamo-bingwa Ufaransa,atachukua usuakni utakoachwa na kocha wa sasa Ottmar hitzfeld.

Klinsmann akiwa na umri wa miaka 43,aliwahi kuichezea bayern munich kati ya 1995 na 1997.Tangazo la Bayern munich limewasangaza wengi hata kocha wa timu ya taifa Joachim Loew aliekuwa msaidizi wa Klinsmann katika kombe la dunia 2006.

Mwenyekiti wa shirikisho la dimba la Ujerumani DFB Theo Zwanziger amesema ni ffuraha ilioje kwa klinsmann kurejea katika dimba la ujerumani.

Kocha mwengine maarufu wa zamani aliefundisha pia Bayern Munich alisema amesangazwa binafsi,kwani hakudhani kuwa Klinsmann angechukua kazi hiyo huko Munich na akaonya kuwa kuteuliwa kwake kuna hatari zake.

Vigogo vya uongozi wa Bayern Münich kama vile Franz Beckenbauer,rais wake Karlheinz rummenigge na meneja Uli Hoeness wakitaka kuwa na kocha maarufu kwa timu hii yenye mastadi kama mfaransa Franck Riberry,mtaliana Luca toni na mjerumani miroslav klose.

Klinsmann ataanza kazi Julai mosi na aliwasili munich jana.

Kwa upande mwengine ,kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani Jens Lehmann aonesha atarudi klabu yake ya zamani Borussia Dortmund kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu.

Kipa huyu anaetapia kulinda lango la Ujerumani katika kombe lijalo la Ulaya hapo juni huko Uswisi na Austria, anasubiri tu kutia saini mkataba na B.Dortmund.Gazeti la Bild la Ujerumani limearifu kwamba Lehmann –kipa wa Arsenal aliewekwa nje ya lango kwa muda mrefu,ameridhia kupokea mshahara mdogo kuliko wa sasa ili arudi tu langoni.

Tugeukie Kombe lijalo la afrika la mataifa linaloanza jumapili ijayo mjini accra Ghana:Litachezwa katika jumla ya viwanja 5 :Accra,Kumasi,Tekoradi,Sekondi na Temale.

Je, Mafiraouni Misri watarudi Cairo na taji lao au wataliacha Accra au litavuka mpaka kuingia jirani Abidjan-Ivory Coast na vipi simba wa nyika-Yaounde-Kameroun ?

Kuna timu za wastani zinazokuja kwa meno ya juu katika dimba la Afrika-timu kama angola ,namibia na hata Mali:

Mastadi wao wameanza kutamba kama vile Flavio Amado-mshambulizi wa angola,mwenyeji wa kombe linalofuatia hili la Ghana 2010.Flavio jinsi alivyo hatari,klabu yake ya Misri Al Ahly, ingali ikimn’gan’gania na haitaki kumuuza.Al Ahly imekataa hodi hodi zote zilizopigwa mlangoni mwake na klabu mbali mbali za Ulaya.Kwavile Fabrice Akwa Maieco amestaafu kutoka timu ya taifa, Angola inayofuatana na jirani zake Afrika Kusini na Namibia,katika kombe hili la Afrika itamtegemea Amado kutamba na kupepea huko Ghana bendera ya COSAFa-shirikisho la dimba la kusini mwa Afrika.

Sudan,mabingwa wa CECAFA-shirikisho la kabumbu la Afrika mashariki na kati, ni timu pekee itakayopepea bendera ya Afrika.

Afrika kusini kwa upande wake, inaongozwa katika kombe hili na mbrazil Carlos Alberto Parreira ambae angependa Bafana Bafana irudie ule ushindi wa 1996 pale kombe hilo lilipoaniwa nyumbani mbele ya mzee Madiba na wakalichukua.Lakini,Bafana Bafana haichezi tena na akina Lucas radebe,Mark Fish au hata Dr.Khumalo.

Tegemeo lao ni Zuma wa Bundesliga na Ben mCcATHY ALIETIA MABAO $ KATI YA != YALIOIONGOZA Afrika kusini katika kombe hili.

Endapo Afrika kusini ikiteleza, vilio vitahanikiza kwamba Parreira alieongoza Brazil kutwaa kombe la dunia, 1994 nchini Marekani, hana lake jambo na an’gatuke.

 • Tarehe 11.01.2008
 • Mwandishi Ramadhan ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CoR3
 • Tarehe 11.01.2008
 • Mwandishi Ramadhan ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CoR3

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com