Michezo mwishoni mwa wiki | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 24.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Michezo mwishoni mwa wiki

Sudan yailaza Ruanda na kuibuka mabingwa wa CECAFA-kombe la Challenge la Afrika mashariki na kati.

Sudan ndio mabingwa wa zamasni na wapya wa kombe la Challenge Cup-kombe la Afrika mashariki na kati.

Waziri wa michezo wa Zanzibar Shamhuna adai Kombe lijalo la Challenge liandaliwe visiwani kuli ngana na jinsi Zanzibar Heroes walivyotamba mwaka huu-lakini jukumu hilo imeshapewa Kenya-sasa itakuaje ?

Ujerumani yawachagua Magdalena Neuner bingwa wa dunia wa Biathlon,Fabian Hambüchen,stadi wa gymnastic na kocha wa timu bingwa ya dunia ya mpira wa mkono –handball Heiner Brand „wanaspoti bora wa mwaka“ wa Ujerumani. Tutawaarifu pia ni timu gani katika Premier League ya Uingereza,La Lioga-Spian na Serie-Itali zimeparamia kileleni mwa Ligi mwishoni mwa wiki.

Kinyan’ganyiro cha kombe la Afrika mashariki na kati-kombe la Cecafa la Challenge Cup lilimalizika jumamosi mjini Dar-es-salaam kwa ushindi wa Sudan, timu pekee katika kanda hii inayoshiriki mwezi ujao katika Kombe la Afrika la mataifa nchini Ghana.

Ruanda ilichachamaa kabisa mbele ya mabingwa hao watetetezi katika finali na timu hizo 2 zikisimama suluhu mabao 2:2, mikwaju ya penalty ikaamua hatima ya mshindi na wakati Ruanda iliitoa Zanzibar Heroes kwa mikwaju ya penalty, mara hii ilikua Sudan ilioangukiwa n a bahati ya kutia mikwaju mingi kimiyani.

Nje ya kombe la Challenge, kocha wa Ujerumani Joachim Loew anaamini kwamba mabingwa wa dunia Itali na makamo bingwa Ufaransa ndizo timu 2 zinazofaa kutumainiwa kutwaa kombe la Ulaya 2008 wakati Spian na Ureno zina uwezo pia kuibuka mabingwa huko Austria na uswisi.

Baada ya kitambo kirefu cha kuwa nje ya chaki ya uwanja kwa kuumia ,nahodha wa timu ya Taifa ya Ujerumani Michael Ballack anataka kufidia kipindi hicho kwa kuibuka mabingwa wa kombe la ulaya la klabu bingwa-champions League na timu yake ya Chelsea pamoja na kuibuka mabingwa wa Ulaya na Ujerumani.

Katika mazungumzo yake na jarida la dimba-Kicker-toleo la kesho, Ballack anataka kurekebisha mambo baada ya miezi 8 ya kutoteremka uwanjani.

Kipa wa timu ya Taifa ya Ujerumani na wa Arsenal London, Jens Lehmann, anazingatia wakati huu alao ombi moja lililomfikia kuihama Arsenal.Kipa huyo wa Ujerumani amekuwa hachezeshwi kulinda lango la Arsenal kitambo sasa kutokana kwanza na kuumia na pili kwa ajili ya kutocheza uzuri langoni.Mwenzake mspain manuel Almunia amekuwa akitamba.Miongoni mwa klabu zinazopiga hodi langoni mwake Lehmann ni Borussia Dortmund.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza,Arsenal wameweza kun’gan’gania usukani wa Ligi ingawa kwa pointi 1 mbele ya mabingwa Manchester united kufuatia ushindi wao wa mabao 2:1 nyumbani dhidi ya Totenham Hotspur.

Katika La Liga-Ligi ya Spain, Real Madrid imetamba kwa bao 1:0 mbele ya mahasimu wao wakubwa nchini-FC Barcelona .Huu ni ushindi wapili tu mnamo miaka 24 wa Real katika uwanja wa FC Barcelona.Kwahivyo, furaha ilioje kwa Real.

Katika Serie A huko Itali, Waargentina 2 :Julio Cruz na Esteban Cambiasso walilifumania lango la mabingwa wa Ulaya na dunia AC Milan na kuwachapa mabao 2:1.Lakini, walikuwa mabingwa wa dunia AC walioufumania kwanza mlango wa Inter, Inter ikiwaambia „kutangulia si kufika“ na vishindo vyenu vya darini sasa vimeishia sakafuni.

Ujerumani imewateua wanaspoti wake wa mwaka 2007: Licha ya kwamba timu ya wasichana ya Ujerumani ilitawazwa mabingwa wa dunia huko China, mwanaspoti wa mwaka hakutoka katika uwanja wa dimba:Bingwa mara 3 wa mchezo wa biathlon Magdalena Neuner alivaa taji la wanawake.Akitoa shukurani zake alisema:

„Nadhani taji la mwanaspoti bora wa mwaka ndilo taji kubwa kwa mwanaspoti nchini Ujerumani.Na hivyo, nina furaha kubwa na ninafurahia sasa taji hilo.“

Nae mwanaspoti bora wa kiume wa mwaka bingwa wa Gymnastics-Fabian Hambüchen alisema,

„Hii ni nishani kubwa niliotunzwa hadi sasa na taji hili litajipatia nafasi nzuri chumbani kwangu:“

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com