Meunier alenga kupata mataji akiwa na Dortmund | Michezo | DW | 16.07.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Meunier alenga kupata mataji akiwa na Dortmund

Thomas Meunier analenga  kupata mataji akiwa  na  Borussia Dortmund katika  msimu wake wa kwanza na klabu hiyo  ya Bundesliga baada  ya  kuhama  kutoka Paris Saint-Germain.

"Iwapo utaangalia ubora wa  kikosi, katika  miaka  ijayo klabu  ni lazima  ishinde kitu tena," mchezaji  huyo  wa  ulinzi  kutoka  Ubelgiji aliliambia shirika  la  habari la  Ujerumani dpa.

UEFA Champions League l BVB v PSG

Thomas Meunier (kulia) akipambana na Thorgan Ha Hazard wa BVB katika pambano la Champions League

"Na tutafanya  hivyo. Mapenzi  yangu kwa  ushindi na  mataji  hayana ukomo."

Meunier , mwenye umri  wa  miaka 28, ameshinda  ligi  ya  Ubelgiji na  kikombe cha  chama  cha  mpira  akiwa  na  Club Brugge  na alipata  mataji  matatu  mfululizo  akiwa  katika  Ligue 1  nchini Ufaransa  pamoja  na  vikombe  kadhaa  akiwa  na  PSG. Mlinzi huyo  wa  kulia  alikuwa  sehemu ya  kikosi  cha  Ubelgiji  ambacho kilimaliza  katika  nafasi ya tatu  katika  kombe  la  dunia  mwaka 2018.

Meunier angependa  kuchelewesha  kuwasili  kwake Dortmund kwa wiki  chache kuweza  kushuhudia  taji  moja  zaidi  akiwa  na  PSG lakini  makubaliano  kumuwezesha yeye  kucheza  katika  michuano ya  fainali  ya  Champions League mwezi  Agosti mjini  Lisbon hayakuweza  kufikiwa.

FIFA WM 2018 Belgien gegen England

Thomas Meunier (kushoto) akipambana na akipambana na mlizi wa timu ya taifa ya Uingereza Danny Rose katika mchezo wa kombe la dunia 2018.

Meunier alitaka kubakia kwa muda PSG

Maafisa  wa  Dortmund walikuwa  tayari, Meunier alisema, lakini mkurugenzi  wa  spoti  wa PSG  Leonardo hakuwa  tayari  kwa  hilo.

"Leonardo  hakuwa  katika  wakati  wowote akitaka  kutafuta makubaliano  na  Dortmund, licha  ya mimi," Meunier alisema. "Alitaka mimi kuitumikia  PSG  bure."

Badala  yake alifahamishwa  kupitia  barua ya  wakili  kukaa  mbali na  viwanja  vya  klabu  hiyo. wakili  wake  alijaribu  kumpatia  yeye nafasi  kwa  ajili  ya  kufanya  mazowezi, kutokana  na  vizuwizi  vya virusi  vya  corona, lakini  jaribio  hilo  lilikataliwa.

"Kisha  nikaambiwa  kwa  simu  kuwa  nisijaribu kuvuka mstari wa yeyote  yule  kwasababu  naweza  kusimulia hadithi  za  kukera hapo  baadaye," Meunier alisema. "Ni  hali  ya  kukosa  uhalisia."

Frankreich Fußball | Pokal | Paris SG vs Dijon

Thomas Meunier akipongezana na Eric Maxim Choupo Moting wakati akiwa na PSG

"Leonardo  aliwaambia waandishi  habari  nchini  France kuwa nimekataa kurefushwa mkataba. Lakini  hiyo  si  sahihi, natak kusema  hilo  wazi."

Meunier anakosoa  pia  uamuzi wa  Ufaransa  na  Ubelgiji kufuta msimu  uliopita  wa  ligi  kwasababu  ya  virusi  vya  corona na  sio kuanzisha  tena  kama  ilivyokuwa  kwa  ligi  zingine  kubwa barani Ulaya.