1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Meloni kukatisha mkutano kutokana na mafuriko Italia

20 Mei 2023

Waziri mkuu wa Italia, Giorgia Meloni ataondoka mapema kabla ya kumalizika kwa mkutano wa mataifa ya G7, kutokana na janga la mafuriko lililosababisha vifo vya watu 14 nchini mwake.

https://p.dw.com/p/4Rc8f
Athari za mafuriko kaskazini mwa Italia
Athari za mafuriko kaskazini mwa Italia Picha: ANDREAS SOLARO AFP via Getty Images

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la AFP likinukuu chanzo kimoja cha kidiplomasia kilichoarifu kuwa Meloni ataondoka jioni ya leo mjini Hiroshima na kurejea Italia.

Mafuriko yaliyosababisha kutokea kwa janga hilo yalitokana na mvua iliyonyesha kwa saa 36 katika mkoa wa Emilia Romagna.  Yanatajwa kuwa ndiyo mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini Italia katika kipindi cha karne moja.

Viongozi wa kundi la G7, wameahidi kumsaidia Meloni ambaye wakati wa mazungumzo, aliwaonesha picha za janga hilo. Rais Emmanuel Macron kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika kuwa Ufaransa iko tayari kutoa msaada muhimu kwa Italia.