1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbio za kucheza kandanda la Ulaya zapamba moto Bundesliga

Bruce Amani
11 Aprili 2022

Kiungo wa Ufaransa Christopher Nkunku ameendeleza makali yake baada ya kufunga bao moja na kutoa pasi ya bao jingine wakati walipowazaba wawaniaji wa nafasi za kandanda la Ulaya Hoffenheim 3 – 0

https://p.dw.com/p/49mqk
Bundesliga - RB Leipzig v TSG 1899 Hoffenheim
Picha: Jan Huebner/IMAGO

Ushindi huo umeyapiga jeki matumaini ya Leipzig kumaliza katika nafasi nne za Kwanza katika Bundesliga huku kukiwa na mechi tano zilizobaki msimu huu.

Nkunku sasa amefunga mabao 17 ya ligi na kutoa assisti 12 wakati Leipzig, ambayo haijapoteza mechi hata moja kati ya nane zilizopita za Bundesliga, ikipinda hadi nafasi ya nne na pointi 51, pointi tatu mbele ya nambari tano Freiburg ambao walishinda 2 -1 dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Fußball Bundesliga |  Eintracht Frankfurt v SC Freiburg | 1:2 durch Nils Petersen
Freiburg waliwazidi maarifa FrankfurtPicha: Jürgen Kessler/Kessler-Sportfotografie/IMAGO

Hoffenheim wako naifasi ya sita na pointi 44. Bayer Levekusen ikiwa katika nafasi ya tatu na pointi 52  ilitoka sare tasa dhidi ya VfL Bochum. Na sasa watawaalika Leipzig Jumapili ijayo.

Cologne huenda ikawa timu bora y amsimu baada ya kuponea chupuchupu kushushwa daraja msimu uliopita. Vijana hao wa kocha Steffen Baumgart walipata ushindi wa 3 -2 dhidi ya Mainz baada ya kutokea nyuma mabao mawili kwa sifuri na kusonga hadi nafasi yxa nane na pointi 43, moja tu nyuma ya nambari sita Hoffenheim na nafasi ya Europa Conf§Erence League. Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa katika mechi hiyo

Katika deby ya Berlin, Union Berlin iliibamiza Hertha Berlin 4 -1 na kuimarisha matumaini yao ya kufuzu kandanda la Ulaya na kuyaharibu matumaini ya watani wao hao wa mjini ya kuepuka shoka la kushushwa ngazi. Hertha wako pointi moja nyuma ya Suttgart ambayo iko nafasi ya 15. Wolfsburg ilipata ushindi wa 4-0 dhidi ya Arminia Bielefeld. Bielefeld sasa wako mbele ya Hertha na tofauti ya mabao. Washika mkia Greuther Fuerth walipigwa 2 -0 dhidi ya Borussia Mönchengladbach.

afp, dpa, reuters, ap