1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaAfrika

Uchimbaji wa lithium Afrika wafichua ubaya wa nishati safi

17 Novemba 2023

Mbio mpya za uchimbaji wa madini ya lithiamu barani Afrika zinachochea ufisadi na kudhuru jamii na mazingira, uchunguzi umebainisha.

https://p.dw.com/p/4Ywm9
Zimbabwe | Uchimbaji wa Lithiamu Goromonzi
Mgodi wa Arcadia nchini Zimbabwe unachukuliwa kuwa mojawapo ya rasilimali kubwa zaidi za mawe ya lithiamu dunianiPicha: Tafadzwa Ufumeli/Getty Images

Katika mgodi unaomilikiwa na china wa uchimbaji madini ya Lithium nchini Namibia, wafanyakazi huko wamekuwa wakilalamika kwa miezi kadhaa kuhusu hali duni ya maisha na mazingira yasio salama ya kufanyia kazi. 

Uchunguzi uliofanywa na wajumbe wa chama cha wafanyakazi wa mgodi nchini humo, katika mgodi wa  Uis mine unaomilikiwa na kampuni ya China ya Xinfeng Investment, uligundua kwamba wachimba mgodi wa ndani wanaishi katika sehemu ndogo iliyo na joto jingi isiyokuwa na maeneo ya kutosha ya kupitishia hewa safi.

Muungano huo wa wafanyakazi pia umekosoa sehemu hizo kukosa maeneo ya faragha kufuatia vyoo na mahala pa kuogea vimewekwa mahala pamoja pa wazi, huku wafanyakazi raia wa China wakiishi sehemu nzuri zilizo na viyoyozi na vyoo vizuri.

Kampuni hiyo ya China pia imedaiwa kukosa kuwa na nguo maalum za kujikinga wakati wa kazi na kutokuwa na mikakati ya usalama kwa wafanyakazi wake.

Gari la kielektroniki.
Kadiri mahitaji ya magari ya umeme yakiongezeka, ndivyo pia mahitaji ya madini ya lithium.Picha: Torsten Sukrow/SULUPRESS.DE/picture alliance

Masuala haya sio pekee yaliyo na utata katika kampuni hiyo ya Xinfeng Investments, Uchunguzi mpya wa uchimbaji madini ya Lithium Africa uliofanywa na shirika moja lisilo la kiserikali la Global Witness lililo na makao yake Uingereza, limeorodhesha madai dhidi ya kampuni hiyo kuanzia kupata idhini ya kuwa na mgodi wa Uis Mine kupitia ufisadi na kwa kuikuza kupitia vibali vilivyokusudiwa kwa wachimbaji madini wadogo wadogo.

Soma pia: Watu waondolewa kwa lazima katika maeneo ya migodi Kongo

Kuiendeleza kampuni hiyo kupitia vibali hivyo, kunamaanisha kampuni hiyo inalipa kiasi kidogo cha fedha na pia kuiruhusu kuvuka baadhi ya kanuni za mazingira.

Mwekeleo wa kutatiza wa ufisadi

Kama ilivyo kwa Namibia, ripoti hiyo pia imeorodhesha visa vya uvunjifu wa haki za binaadamu, ufisadi, ukosefu wa makazi, maeneo yasio salama ya kufanyia kazi katika migodi ya uchimbaji madini ya Lithium katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hata Zimbabwe.

Sikiliza pia: 

Mtu na Mzingira: Uchimbaji wa madini ya Kinywe rafiki kwa mazingira

Mtafiti mkuu wa shirika hilo la Global Witness Colin Robertson amesema kwa kuangalia miongo kdhaa iliyopita, sekta ya uchimbani madini Afrika imekuwa ikihusishwa na masuala ya ufisadi na jamii imekuwa mara zote ikikosa kufaidika.

Amesema kile walichogundua ni kwamba katika uchimbaji wa madini ya Lithium mambo yanaendeshwa katika mkondo huohuo jambo linalotoa wasiwasi mkubwa.

Madini hayo ni muhimu katika kutengenezea betri za simu pamoja na magari. Betri kama hizo pia ni muhimu sana kwa  kuhifadhi nishati inayozalishwa kupitia nishati ya jua au upepo.

Zimbabwe | Uchimbaji wa Lithium Buhera
Zimbabwe imepiga marufuku usafirishaji wa lithiamu mbichi nje ya nchi - kwenye kiwanda hiki, ore ghafi iliyosagwa huchakatwa na kuwa mkusanyiko.Picha: Shaun Jusa/Xinhua/picture alliance

Madini ya wakati ujao

Kwa sasa usambazaji wa Lithium unafanywa na mataifa kama Australia, Chile na China ambao kwa pamoja walizalisha asilimia 90 ya vyuma vyepesi mwaka 2022, lakini kwa karibu asilimia 5 ya akiba ya madini hayo, Afrika bado ina uwezo mkubwa  ambao bado nafasi yake haijatumiwa vizuri.

Tanzania yasaini mikataba ya madini ya nadra na makampuni ya Australia 

Kwa sasa ni Zimbabawe na Namibia tu zilizosafirisha Lithium Ore huku miradi iliyo katika nchi kama vile Congo, Mali, Ghana, Nigeria, Rwanda na Ethiopia ikiwa bado inaendelea.

Wakati uhitaji wa madini hayo ukiendelea kuwa mkubwa, huenda matumizi yake yakaongezeka ifikapo mwaka 2040 hii ikiwa ni kulingana na makadirio ya shirika la kimataifa la nishati.

Hii inasababisha nchi zilizo na uchumi mkubwa pamoja na makampuni ya kimataifa yakiwa mbioni kufikia madini ya Lithium barani Afrika, na hiyo ndio inaongeza visa vya ufisadi kushamiri barani humo na wakazi wa maeneo kunakopatikana madini hayo kukosa kufaidika na rasilimali hiyo.

Ufafanuzi:Kwanini Niger ni muhimu kwa mataifa ya magharibi?