1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo kati ya M23 na serikali bado yanaendelea

11 Desemba 2012

Mazungumzo baina ya wajumbe wa kundi la waasi la M23 na wale wa serikali kuu ya DRC yaliyoanza mjini Kampala mji mkuu wa Uganda jumapili iliyopita yanaonekana kuwa yamekwama.

https://p.dw.com/p/16zlD
Waasi wa M23 bado wamo kwenye meza ya mazungumzo na Serikali
Waasi wa M23 bado wamo kwenye meza ya mazungumzo na SerikaliPicha: Reuters

 Ujumbe wa viongozi wa  kidini kutoka DRC ukiongozwa na Mufti wa waislamu wa Kongo akiwa pia mwenyekiti wa muungano wa madhebu ya Congo kwa ajili ya amani Sheikh Abdallah Mangala Luaba, ulikutana kwa mazungumzo na kiongozi wa madhehebu ya Uganda kwa uwepo wa wajumbe wa mashirika ya kiraia wa nchi zote mbili, kujadili hali ya usalama mashariki mwa DRC.
John Kanyunyu alizungumza na Sheikh Abdallah Mangala, ambaye anatuambia
kwanini walikutana.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: John Kanyunyu

Mhariri: Saumu Yusuf