1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa mambo ya nje wa BRICS wakutana nchini India

14 Mei 2026

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka kundi la BRICS, wameanza leo mkutano wa siku mbili mjini New Delhi, India huku jumuiya hiyo ikikabiliwa na mgawanyiko kuhusu vita nchini Iran na kupanda kwa bei ya nishati

https://p.dw.com/p/5DknI
BRICS-mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje 2026 | New Delhi
Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la BRICS katika picha ya pamoja mjini New Delhi, India, mnamo Mei 14Picha: Manish Swarup/AP Photo/picture alliance

Mkutano huo unawaleta pamoja wanadiplomasia kutoka Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini pamoja na nchi wanachama wapya.

Katika mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi aliyahimiza mataifa ya  BRICS kuzilaani Marekani na Israel kwa kile alichokiita "uchokozi wao usio halali" dhidi ya Tehran.

"Tuko tayari kupigana kwa kutumia kila kitu tulichonacho kwa ajili ya kutetea uhuru wetu na ardhi yetu, lakini pia tuko tayari kufuata na kusimamia diplomasia. Kama ambavyo nimekuwa nikisema wakati wote halitapatikana suluhisho la kijeshi katika kutatua chochote kinachohusiana Iran.

Araghchi amesema ni muhimu kwa wote kuongeza juhudi za kukomesha hali ya ubora na kutokujali kwa upande wa Marekani, dhana aliyosema haina nafasi katika ulimwengu wa leo.