1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Matokeo ya awali yawapa ushindi wafuasi wa Imran Khan

Iddi Ssessanga
9 Februari 2024

Wafuasi wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan alieko gerezani Imran Khan walikuwa wanaongoza katika matokeo ya uchaguzi wa Pakistan kwa zaidi ya viti 100.

https://p.dw.com/p/4cDHZ
Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan.Picha: DW

Chombo cha habari cha Geo News kimesema wagombea huru, ambao wengi wao ni watiifu kwa Khan, wameshinda viti 47 kati ya 106 vilivyotangazwa kati ya jumla ya viti 265 vilivyogombaniwa katika uchaguzi wa Alkhamis (Februari 8).

Soma zaidi: Mahakama ya Uchaguzi Pakistan yaamuru kuharakishwa matokeo

Kufikia saa 5:00 asubuhi ya Ijumaa (Februari 9), Tume ya Uchaguzi ya Pakistan (ECP) ilikuwa imetangaza matokeo rasmi ya viti 70, ambapo wagombea huru walikuwa na viti 24.

Soma zaidi: Pakistan yaanza kuhesabu kura baada ya uchaguzi kukamilika

Chama cha Pakistan Peoples Party cha Bilawal Bhutto Zardari, mtoto wa waziri mkuu aliyeuawa Benazir Bhutto, pia kilikuwa na viti 24, huku chama cha Pakistan Muslim League-Nawaz cha waziri mkuu wa zamani, Nawaz Sharif, kikiwa na viti 18.

Khan yuko jela na chama chake cha Pakistan Tahreek-e-Insaf kilizuiwa kushiriki uchaguzi na hivyo wafuasi wake walishiriki kama wagombea binafsi.