1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matiangi: Tumejiandaa kuilinda Kenya wakati wa uchaguzi

14 Julai 2022

Maafisa wa usalama wanahitimisha mikakati ya usalama zikiwa zimesalia siku 25 Kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika Kenya Ili kuimarisha operesheni hizo,

https://p.dw.com/p/4E9Dt
Kenia Symbolbild Wahlen und Social Media
Picha: AFP/T. Karumba

Kwenye kikao cha pamoja cha wakuu wa usalama wa kitaifa na kaunti wa idara mbalimbali, waziri wa usalama wa taifa Fred Matiangi alielezea kuwa ana imani wamejiandaa kikamilifu.

Kimesalia kikao kimoja cha maandalizi ya usalama wa uchaguzi kilichopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Wakuu hao wa usalama wamekuwa wakifanya mikutano na maafisa wa tume ya uchaguzi ili kujiandaa kwa lolote ukizingatia usimamizi wa mihadhara.

Operesheni hizo zinajumuisha pia uangalizi katika vituo vya kupigia kura kulingana na nyenzo zilizopo ili vifaa vya uchaguzi visafirishwe ipasavyo.

Usalama unaimarishwa kampeni zazidi kupamba moto

Yote hayo yakiendelea, Mgombea wa urais wa Chama cha UDA kupitia muungano wa Kenya Kwanza anaandamwa na shutuma za kutumia lugha ya udhalilishaji akiwa kwenye  kampeni.

Akitumia jukwaa la kisiasa wakati wa kuomba kura Ruto amesema kuna mpango wa kubadili katiba, lakini kipaumbele cha wananchi kwa sasa ni kubadili uchumi wa taifa hilo la Afrika mashariki.

Kwa upande wake, Azimio la Umoja One Kenya inanadi sera eneo la pwani. Mgombea mwenza wa Urais Martha Karua anasisitiza kuwa hakuna atakayeonewa watakapoingia madarakani.

Amesema mgombea wa Azimio la Umoja Kenya Raila Odinga amedhamiria kuborosha uchumi wa nchi hiyo na kuhakikisha maisha ya wananchi yanaimarika.

Tume ya uchaguzi ya kenya IEBC inaendelea na kampeni ya kutoa elimu kwa wapiga kura. TM,DW Nairobi.

Juhudi za amani kabla ya uchaguzi Kenya