Mashambulizi ya droni Kongo yatishia juhudi za amani
14 Machi 2026
Matangazo
Msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba kundi hilo litaendelea kuonyesha nia thabiti kwa juhudi za amani ikiwa jeshi la Kongo litaepuka kushambulia maeneo yao na kuwauwa viongozi wao, wanajeshi na raia wasiokuwa na hatia.
Kwa upande wake, msemaji wa serikali ya Kongo Patrick Muyaya amesema serikali inachunguza shambulizi la wiki hiii lililomuuwa mfanyakazi wa shirika la misaada raia wa Ufaransa, lakini hakufafanua zaidi kuhusu mashambulizi mengine ya droni.
Muyaya ameilaumu M23 kwa kukiuka makubaliano ya kusitishaji mapigano, lakini akasema kuwa upande wa serikali ungependa kusisitiza tena kujitolea kwao kuheshimu makubaliano hayo ya kusitisha mapigano pamoja na makubaliano mengine.