Mashabiki 22 wauwawa katika dimba Ivory Coast | Michezo | DW | 30.03.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Mashabiki 22 wauwawa katika dimba Ivory Coast

Ujerumani yailaza Liechtenstein kwa mabao 4:2.

MichaelBallack-nahodha wa Ujerumani.

MichaelBallack-nahodha wa Ujerumani.

Mashabiki 22 wafariki dunia mjini Abidjan, pale Tembo wa Ivory Coast walipowalipo wakanyaga jana Malawi kwa mabao 5-0 katika kinyanganyiro cha kuania tiketi ya kombe lijalo la dunia-

Kombe la dunia mwakani nchini Afrika Kusini laweza kuamua iwapo pia michezo ya olimpik ifanyike barani afrika-asema rais wa Halmashauri kuu ya olimpik ulimwenguni (IOC ).

Ujerumani, yatamba kwa mabao 4-0 dhidi ya chipukizi Liechtenstein katika kanda ya ulaya ya kufuzu kwa Kombe la dunia na .

Ama katika kanda ya Amerika Kusini,Argentina ikiongozwa na kocha Maradona yatamba wakati Brazil yateleza.

Tuanze na kinyanganyiro cha kufuzu kwa kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika kusini katika kanda ya Afrika,Ulaya na Amerika kusini.

katkka ka nda ya Afrika msiba mkubwa ulizuka jana pale hadi mashabiki 22 walipuwawa uwanjani Abidjan,Ivory Coast pale ukuta ulipoanguka na kuzuka mkanyagano Ivory Coast ilipocheza na Malawi.Ivory Coast ikicheza na stadi wake alietia pekee mabao 2-didier drogba ,ilitimua Malawi kwa mabao 5:0.Nigeria,lakini iliteleza mbele ya Msumbiji.

Mashabiki 22 walifariki dunia jana pale maalfu ya mashabiki wa nnyumbani waliposheheni katika Uwanja wa Houphouet-Boigny(Houfet Bwanyi) mjini Abidjan kuwaangalia tembo wao wakiikanyaga Malawi.

Waziri wa ndani wa Ivory Coast, Desire Tagro, alikiambia kituo cha TV cha Ivory Coast , kuwa kusheheni kupita kiasi kwa mashabiki, kulizusha kihoro uwanjani na hii ikaongoza kukanyagana kwa watu na vifo.Mashabiki 100 wengine walijeruhiwa.

Polisi ilijaribu kudhibiti makundi ya mashabiki ingawa kuna taarifa zinazodai kwamba, polisi hao walimwaya hewa ya kutoa machozi na hivyo kuzidisha hofu na patashika.

Msongamano katika mechi za mpira barani Afrika, ni kisa kinachotokea mara kwa mara .Uuzaji tiketi wa kupita kiasi na kutodhibi makundi ya mashabiki ipasavyo, kukichangia mno katika balaa kama hili la jana.

Mashabiki 13 waliuwawa huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hapo septemba mwaka jana, baada ya machafuko kuzuka kutokana na tuhuma za kuroga na uchawi katika dimba. Mashabiki wengine 23 walifariki nchini Sudan,Julai mwaka jana kufuatia msongamano wakati wa mechi moja nchini humo. na hivi ni visa vya karibuni tu.

Ama katika viwanja vya dimba lenyewe, mbali na Ivory Coast kuizaba malawi mabao 5 bila jibu jana, Nigeria -super eagles ilitoka mikono mitupo mjini Maputo ilipoondoka sare tu 0:0 na wenyeji mamba wa Msumbiji. Matokeo hayo yameuzusha hofu tena kwamba Nigeria yaweza ikalikosa Kombe lijalo la dunia mwakani nchini Afrika kusini kama ilivyolikosa kombe lililopita la dunia hapa Ujerumani 2006.

Mara ile Angola iliipiku Nigeria na kuja Ujerumani.Na sasa jirani zao mamba wa msumbiji waliopo nafasi ya 93 ya ngazi ya dimba la dunia ,wamewatia munda Super eagles katika uwanja wa Machava, mjini maputo.Nigeria hata hivyo ilitamba mapambano yake yaliotangulia kwa kuwalaza wenyeji bafana Bafana,Sierra Leone na Guinea ya Ekweta.

Ama jirani zao Ghana au Black Stars ,walilifumania dakika ya kwanza tu lango la Benin mjini Kumasi.Lakini hodi hodi zao zaidi walizopiga katika lango la benin hazikuitikiwa.

Mabingwa wa afrika Misri, walikiona kilichomtoa kanga manyoya baada ya kuongoza kwa bao 1 nyumbani Cairo. Chipolopolo -risasi za zambia, mwishoe ziliwapata pale Francis Kasonde alipolifuta bao la Amr Zaki.

Je, Harambee Stars-Kenya ilichezaji na Watunisia mjini Nairobi ? Kenya ilizabwa mabao 2:1 na Tunisia na sasa ina miadi duru ijayo na Nigeria.Katika kanda ya Ulaya ya kuania tiketi za Kombe lijalo la dunia, Ujerumani ilipasi mtihani wake wa kwanza jumamosi kati ya mitatu kabla kukata tiketi yake ya Kombe lijalo la dunia nchini Afrika Kusini.

Ushindi wa mabao 4-0 wa Ujerumani dhidi ya Liechtenstein majuzi si ishara kwamba Ujerumani itapata mteremko jumatano hii itakapoingia tena uwanjani na Wales.Ujerumani ingali bado pointi 4 mbele kuliko Urusi yenye miadi nayo hapo oktoba.Urusi ina miadi keshokutwa na Liechetenstein na bila ya shaka itaondoka kama Ujerumani na pointi 3.

Moja kati ya mabao 4 ya Ujerumani dhidi ya Liechtenstein, lilitiwa na Lukas Podolski anaeichezea wakati huu Bayern Munich.

Podolski aliueleza mpambano wa jumamosi baada ya ushindi hivi:

"ukishinda na ukatia bao,basi daima mambo huwa mazuri.Kabla mchezo huu, tulisema tuna nia ya kushinda mechezo 2.Leo tumeshinda wa kwanza kati ya michezo 3 na jumatano ijayo ufuate ushindi mwengine."

Ama kocha wa Ujerumani, Joachim Loew aliueleza mchezo wa jumamosi na Liechtenstein hivi:

"Tulijitahidi kuanza vyema mchezo na vipindi vyote 2 tulipata nafasi kadhaa za kutia magoli na tulitia kasi usoni.Mwishoe, naweza kusema ulikuwa mwsanzo mzuri kwa mechi zotze 2."

Jumatano hii Ujerumani ikicheza na Wales,ndipo itakapobainika wazi zaidi iwapo ujerumani itaipiku urusi hapo oktoba na kutia tiketi yake ya kwenda Afrika Kusini juni mwakani.

Mwishoe, michezo ya olimpik ya majira ya kiangazi imefanyika katika mabara yote isipokuwa Afrika.Rais wa Halmashauri kuu ya olimpik ulimwenguni (IOC) mbelgiji Jacques Rogge ametoa leo ishara huko Wellington,New Zealand kwamba kombe la dunia la dimba mwakani nchini Afrika Kusini ,laweza likatilia nguvu nafasi ya bara la Afrika kuandaa michezo ya olimpik.Akasema rais huyo wa IOC,

"Tungependa kuona michezo ya Olimpik inaandaliwa katika mabara yote."