1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yazingatia kuipa Ukraine makombora ya masafa marefu

29 Septemba 2025

Marekani inazingatia ombi la Ukraine la kupata makombora ya masafa marefu aina ya Tomahawk kwa juhudi zake za kukabiliana na wavamizi wa Urusi. Haya yamesemwa jana na naibu rais JD Vance.

https://p.dw.com/p/51DdK
Marekani  Glendale 2025 | JD Vance
Naibu rais wa Marekani JD VancePicha: Ross D. Franklin/AP Photo/dpa/picture alliance

Katika mahojiano na shirika la habari la Fox, Vance amesema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameitaka Marekani kuuzia mataifa ya Ulaya makombora hayo ambayo yatayatuma kwa nchi yake.

Pia ameongeza kuwa Rais Donald Trump atafanya maamuzi ya mwisho kuhusu iwapo ataruhusu makubaliano hayo.

Trump aghadhabishwa na ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa Putin

Katika siku ya nyuma, Trump alikataa ombi la Ukraine la matumizi ya makombora ya masafa marefu lakini amekua akighadhabishwa na hatua ya Rais wa Urusi ya kukataa kufikia makubaliano ya amani.

Mjumbe maalum wa Marekani nchini Ukraine, amesema Trump amedokeza kuwa Kyiv sasa inapaswa kuwa na uwezo wa kufanya mashambulizi ya masafa marefu dhidi ya Urusi.