1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO : Waliokufa kwa mripuko waongezeka

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCG7

Mripuko katika ghala la silaha kwenye mji mkuu wa Msumbiji umeuwa watu 96 wengi wao wakiwa ni watoto huku kukiwa na hofu ya kuzuka milipuko zaidi kutokana na kupanda kwa hali ya joto.

Waziri wa Afya Ivo Paulo Garrido ametangaza siku tatu za maombolezo kwa wahanga wa mripuko huo uliopelekea pia kujeruhiuwa kwa zaidi ya watu 400.

Kupanda kwa hali ya hewa ya joto kunadhaniwa kuwa ndio sababu ya miripuko hiyo ya mabomu na silaha.Miripuko hiyo iliruka hadi nyumba za karibu na kuziteketeza kadhaa pamoja na kusababisha watu kukimbia kwa hofu.Majengo yalioko umbali wa kilomita 10 pia yameathiriwa na miripuko hiyo.

Waakazi wameonywa kutokaa kwenye nyumba zao kwa siku saba zijazo kutokana na wasi wasi wa kuzuka kwa miripuko mengine.