Mapigano yazuka upya Mogadishu | Matukio ya Afrika | DW | 25.02.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Mapigano yazuka upya Mogadishu

Vikosi vya serikali ya mpito na vya Umoja wa Afrika vyaendelea kupambana na wapiganaji wa al Shabaab. Wakaazi wa Mogadishu walazimika kubakia ndani ya nyumba zao wakihofia maisha yao

default

Wanajeshi wa Somalia wakipiga doria Mogadishu

Mapigano mapya yamezuka mjini Mogadishu Somalia hii leo wakati vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya mpito ya nchi hiyo na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika, AMISOM, vikiendelea na operesheni dhidi ya wapiganaji wa kundi la al Shaabab wenye mafungamano na kundi la kigaidif la al Qaeda.

Afisa wa jeshi la serikali, kanali Mohamed Adan, amesema kwamba vifaru vya kijeshi vya kikosi cha serikali ya mpito na AMISOM vimesonga mbele na kuyateka maeneo muhimu yaliyokuwa yakidhibitiwa na al Shabaab katika wilaya za Holwadad na Wardhigley, kusini mwa mji mkuu Mogadishu.

Wakaazi katika maeneo hayo wamesema wameshindwa kutoka nje ya nyumba zao leo huku mapigano makali zaidi yakiripotiwa kutokea katika barabara ya Wadnaha, eneo muhimu ambalo wapiganaji wana kambi zao.