1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yaripotiwa Sudan licha ya vikwazo vya Marekani

Amina Mjahid
3 Juni 2023

Mapigano kati ya pande mbili hasimu za kijeshi yanaendelea kuripotiwa mjini Khartoum licha ya Vikwazo vilivyowekwa na Marekani baada ya kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

https://p.dw.com/p/4S9d7
Sudan, Khartoum | Anhaltende Kämpfe
Picha: AFP via Getty Images

Mapigano yameripotiwa pia mjini Omdurman na Mashariki mwa mji wa Khartoum. 

Kwa takriban wiki 7 vita kati ya Jeshi la taifa hilo na wanamgambo wa vikosi vya RSF vimepamba moto mjini Kahrtoum na eneo la Magharibi mwa Darfur licha ya juhudi za mara kwa mara za kujaribu kusitisha mapigano. 

Barazala la Usalama lataka vita visitishwe Sudan

Vita hivyo vimesababisha vifo vya watu zaidi ya 700 na wengine zaidi ya milioni moja kukimbilia nchi jirani kama Misri Chad na Sudan Kusini. Wiki ijayo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken anatarajiwa kufika Saudi Arabia kujadili masuala ya ushirikiano wa kimkakati na masuala mengine ya kikanda na kidunia ikiwemo mzozo wa Sudan. 

Mataifa hayo mawili yalisimamia makubaliano yaliyofeli ya kusitisha mapigano kati ya pande mbili hasimu za kijeshi nchini Sudan.