1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano kati ya jeshi la kundi la RSF yaendelea Sudan

Daniel Gakuba
15 Aprili 2023

Jumuiya ya kimataifa imehimiza wanajeshi wa Sudan na kikosi maalumu cha wanamgambo, RSF kuacha mapigano, huku uhasama baina ya pande hizo ukiiweka Sudan katika hali tete.

https://p.dw.com/p/4Q8b2
Sudan Khartum | Kämpfe zwischen Armee und Milizen
Picha: MOHAMED NURELDIN ABDALLAH/REUTERS

Kikosi maalumu cha wanamgambo cha Rapid Support Forces, RSF cha nchini Sudan kimedai kuwa kinadhibiti ikulu ya rais, makao makuu ya jeshi na uwanja wa ndege wa mji mkuu, Khartoum, katika kile kinachoonekana wazi kuwa jaribio la mapinduzi.

Hata hivyo, jeshi la nchi hiyo limesema linapambana na RSF katika vituo inavyodai kuvidhibiti, zikiwemo kambi mbili za jeshi za Merowe na el-Obeid.

Milio ya silaha nzito nzito imesikika katika maeneo mengi ya Sudan, ambapo kikosi cha RSF kimesema kilijitetea baada ya kushambuliwa kwanza na jeshi.

Saudi Arabia imefuta safari za ndege zake kutoka na kuingia Sudan, baada ya kusema kuwa ndege yake moja imekumbwa na mkasa kwenye uwanja wa Khartoum.

Mataifa na taasisi mbalimbali za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Marekani, Urusi, na Umoja wa Mataifa yamezitaka pande zinazohasimiana nchini Sudan kuacha mapigano mara moja.

Chanzo: RTRE