Maoni ya wahariri. | Magazetini | DW | 23.07.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Maoni ya wahariri.

Wanajeshi wa Ujerumani sasa wanapambana na taliban ana kwa ana nchini Afghanistan.

default

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung.

Maafisa wa serikali ya Ujerumani wamethibitisha kwamba wanajeshi wa nchi hii waliopo nchini Afghanistan sasa wanapambana ana kwa ana na wapiganaji wa kitaliban kaskazini mwa nchi hiyo.Na waziri wa ulinzi Franz Josef Jung amekiri kwamba majeshi ya Ujerumani yanakabiliwa na changamoto.

Wahariri wa magazeti takriban yote ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya hali ya nchini Afghanistan.

Hali ni mbaya anasema mhariri wa gazeti la Neue Osnabrücker Zeitung. Mhariri huyo anaeleza kuwa mambo yamekuwa yanaenda mrama katika muda wa miaka minane iliyopita, tokea majeshi ya kimataifa yaingie nchini Afghanistan. Anasema serikali ya Ujerumani pia inapaswa kulaumiwa kwa sababu ya ukaidi wake.Ujerumani imekuwa inakataa kuyasaidia majeshi ya nchi nyingine za Nato, kuwazuia wapiganaji wa kitalibani kusini mwa nchi hiyo na badala yake Ujerumani imekuwa inang'ang'ania shughuli za ujenzi na mafunzo ya polisi kaskazini mwa Afghanistan.

Mhariri wa gazeti la Neue Osnabrücker anasema majeshi ya Ujerumani yamo ndani ya mtumbwi uliotoboka katika vita dhidi ya wataliban.

Gazeti la Hannoversche Allgemeine linatahadharisha juu ya mabadiliko yanayoweza kutokea katika hisia za watu endapo operesheni inayofanyika sasa itachukua muda mrefu.

Mhariri wa gazeti hilo anasema kwa kadri operesheni hiyo itakavyochukua muda mrefu ambapo bila shaka, patatokea vifo, na madhara mengine, vivyo ndivyo hisia za wananchi wa Afghanistan zinatakavyoanza kubadilika.Mtazamo wa kuyaunga mkono majeshi ya Ujerumani utaanza kunyauka miongoni mwa wananchi hao.


Mhariri wa gazeti la Haonnoversche Allgemeine pia anatahadharisha juu ya madhara ya kuuawa kwa raia. Anasema vifo vya raia vitajenga umaaruf wa taliban na hivyo kuwawezesha kupata wapiganaji wapya. Kutokana na hali hiyo, mhariri anasema majeshi ya Ujerumani na ya Afghanistan yanapaswa kuwa na uangalifu mkubwa la sivyo ,lengo linalopiganiwa halitafikiwa, yaani kuleta usalama na kuijenga Afghanistan upya.

Gazeti la Cellesche Zeitung linamtaka waziri wa ulinzi wa Ujerumani bwana Jung atambue hali halisi nchini Afghanistan. Gazeti hilo linauliza jee waziri huyo anahofia kutoweka kupachuka kwa mshikamano wa wananchi wa Ujerumani wakati ambapo uchaguzi mkuu unakaribia nchini ?

Mhariri wa gazeti la Cellesche anasema wananchi wa Ujerumani tayari wana wasiwasi juu ya vifo vya wanajeshi wao na raia wa Afghanistan.

Hatahiyvo gazeti la Sächsiche Zeitung linasema kuondoa majeshi Afghanistan kutakuwa na maana ya kusalimu amri mbele ya taliban na kuifanya nchi hiyo kuwa kambi ya kutayarishia mashambulio ya kigaidi.

Mwandishi/Mtullya Abdu.

Mhariri./

Deutsche Zeitungen.