Maoni ya wahariri juu ya ugaidi | Magazetini | DW | 24.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya ugaidi

Wahariri wa magazeti wanatoa maoni juu ya juhudi za kupambana na ugaidi na juu ya aliekuwa Kansela wa Ujerumani Helmut Schmidt

Ulinzi mkali mjini Brussels

Watoa heshima za mwisho kwa Helmut Schmidt

Gazeti la "Schwabische linazungumzia juu ya hatua zilizochukuliwa nchini Ubelgiji ili kupambana na ugaigi. Mhariri wa gazeti hilo anatilia maanani kwamba shule ,maduka na baadhi ya shughuli za usafirishaji zimefungwa. Mhariri huyo anaeleza kuwa hatua hizo zimechukuliwa ili kuwasaka magaidi wanaotuhumiwa kuhusika na mashambulio ya mjini Paris.

Uzembe wa polisi

Gazeti la "Schwabische" linauliza kulikoni nchini Ubelgiji?. Mhariri wa gazeti anajibu kwa kusema kuwa Ugelgiji inaugua maradhi yanayotokana na unyama uliofanywa na nchi hiyo wakati wa ukoloni nchini Kongo.Dalili za maradhi hayo pia zilionekana katika utobwe uliojitokeza baada ya polisi wa Ubelgiji kuwezesha kupangwa kwa shambulio la kigaidi karibu na makao makuu ya jumuiya kijeshi ya NATO mjini Brussels.

Mhariri wa gazeti la "Rhein-Neckar" anasema ni kosa kuzilaumu idara za usalama za nchini Ubelgiji kwa mashambulio ya kigaidi yaliotokea mjini Paris. Mhariri wa gazeti hilo anasema wakati viongozi nchini Ujerumani wanatuhumu kuwamo magaidi miongoni mwa wakimbizi, watu wanapuuza ukweli uliojitokeza mwishoni mwa wili iliyopita, kwamba ugaidi umeshajijenga barani Ulaya. Anasema magaidi wa dola la kiislamu siyo maadui wanaotokea nje ya Ulaya, bali wamo ndani ya Ulaya.

Helmut Schmidt atakumbukwa daima

Watoa heshima za mwisho kwa Helmut Schmdit

Watoa heshima za mwisho kwa Helmut Schmdit

Gazeti la "Bild" linatukumbusha kwamba kifo cha aliekuwa Kansela wa Ujerumani magharibi Helmut Schmidt kiliwagusa mamilioni ya watu wa marika yote. Mhariri wa gazeti hilo anasema , inaonekana kana kwamba Schmidt ameondoka na sehemu ya historia ya Ujerumani.

Schmidt alikuwa Kansela alieshiriki kwa uthabiti wote katika juhudi za kuitatua migogoro ya dunia na pia alipambana na ugaidi kwa nguvu zote. Mhariri wa gazeti la "Bild" ameikariri kauli ya Schmidt kwamba mtu anapaswa kuulinda uhuru wake.

Naye mhariri wa gazeti la "Flensburger" anasema ,Helmut Schmidt ataendelea kuwa maarufu hata baada ya kuiaga dunia. Sababu ni kwamba aliyapitisha mamuzi yatakayomfanya akumbukwe daima.

Mabadiliko ya mfumo wa siasa Argentina

Mhariri wa gazeti la "Die Rheinpfalz" anasema kuchaguliwa kwa mgombe wa wahafidhina katika uchaguzi wa Rais nchini Argentina, kunawakilisha siyo tu kuondolewa kwa utawala wa mrengo wa kisoshalisti.

Mhariri huyo anatilia maanani kwamba mfumo wote wa kisiasa nchini humo utabadilika.Mhariri wa "Die Rheinpfalz" anasema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Argentina ilikwama kiuchumi na umasikini uliongezeka.Pamoja na hayo uhalifu na biashara ya mihadarati ilikithiri.

Gazeti linaeleza kwamba hayo yote yaliweza kutokea kutokana na utawala wa Rais wa Kirchner" .Kasoro hizo ndizo zilizowafanya watu wengi wa Argentina watake mabadiliko ili kuiondoa sera ya kujinufaisha na ya kujijazia mifuko.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com