MANU yaendeleza ushindi katika Premier League | Michezo | DW | 29.12.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

MANU yaendeleza ushindi katika Premier League

Manchester United imezidi kujichimbia kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza pamoja na jana kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Birmingham City.

default

Wachezaji wa Manchester United wakishangilia katika moja ya mechi walizoshinda

Sare hiyo imeifanya Manchester United kufikisha michezo 18 mfululizo bila ya kushindwa, huku ikiwa na pointi 38 sawa na mahasimu wa mji mmoja, Manchester City, lakini MANU wakiongoza kwa mabao ya kufunga. Hata hivyo, MANU wamecheza mechi chache zaidi ya City ambayo imecheza mechi 20.

Hiyo jana Manchester City iliichabanga Aston Villa mabao 4-0, ambapo mshambuliaji wa kitaliana, Mario Baloteli, alipachika mabao 3-0 pekee yake.

Arsenal inayokamata nafasi ya tatu leo inapambana na Wigan Athletic, baada ya juzi kuichapa Chelsea mabao 3-1. Chelsea, kwa upande wao, leo watajaribu kumtuliza shetani wao kichwani pale watakapopambana na Bolton Wanderers.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters

Mhariri:Othman Miradji