MANU kileleni Premier league
27 Desemba 2010Matangazo
Mabao yote ya MANU yaliwekwa wavuni na Dimitar Berbatov. Katika mechi nyingine, Carlos Tevez aliliweka pembeni jinamizi la kutaka kuihama Manchester City, pale alipopachika mabao 2 kati ya 3 ambayo Manchester City iliichapa Newcastle United.
Tottenham Hotspur ikiwa nyumbani iliichapa Aston Villa mabao 2-1, huku Blackburn Rovers ikilambishwa mchanga nyumbani kwa kukandikwa mabao 2-0 na Stoke City.
Leo kuna kivumbi, pale Arsenal itakapopambana na mabingwa watetezi Chelsea.
Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters
Mhariri:Josephat Charo