1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man City wasaka fainali yao ya kwanza Champions League

3 Mei 2021

Huenda kukashuhudiwa fainali mbili za mashindano makubwa Ulaya yakizikutanisha timu zote za England katika kipindi cha miaka mitatu.

https://p.dw.com/p/3suWK
Fußball | Champions League - Halbfinale - Paris St. Germain vs Manchester City
Picha: Dave Winter/BPI/Shutterstock/imago images

Huenda kukashuhudiwa fainali mbili za mashindano makubwa Ulaya yakizikutanisha timu zote za England katika kipindi cha miaka mitatu.

Hii ni kwa kuwa Manchester City na Chelsea wako katika nafasi nzuri za kuweza kufuzu kwenye fainali ya Champions League huku Manchester United wakiwa wanaonekana kuwa watatinga fainali ya Europa League na huenda wakapambana na Arsenal kwenye fainali hiyo iwapo the Gunners watakapindua kipigo cha 2-1 walichopewa na Villareal wiki iliyopita.

Champions League | Real Madrid vs Chelsea
Christian Pulisic (kulia) akimkabili Marcelo (kushoto)Picha: Angel Martinez/Getty Images

Mwaka 2019 Liverpool walipowalaza Tottenham Hotspur kwenye fainali ya Champions League, Chelsea walikuwa wametoka kuwafunga Arsenal katika fainali ya Europa League huko Baku.

Sasa hapo Jumanne Manchester City watakuwa wenyeweji wa Paris Saint Germain huku wakiwa wanaingia kwenye mtanange huo wakiwa na uongozi wa 2-1 walioupata huko Paris na Jumatano Chelsea watakuwa wanawaalika Real Madrid baada ya sare yao ya bao moja katika mechi ya kwanza.