1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPapua New Guinea

Mamia wahofiwa kufa kwa maporomoko Papua New Guinea

25 Mei 2024

Mamia ya watu wanahofiwa kufa kutokana na maporomoko ya udongo katika kijiji kimoja kilichopo kwenye eneo la milima la Papua New Guinea.

https://p.dw.com/p/4gHSA
Papua-New Guinea, Kaokalam |
Picha iliyotolewa Ijumaa, Mei 24, 2024, inaonyesha eneo ambapo kulitokea maporomoko ya ardhi katika kijiji cha Kaokalam kwenye jimbo la Enga, kilomita 600 kaskazini-magharibi mwa Port Moresby, Papua New Guinea.Picha: Ninga Role/AAP/IMAGO

Kijiji cha Yambili kilichopo kwenye eneo hilo kilifunikwa kabisa na udongo limesema gazeti la eneo hilo la Post Courier hii leo.

Vijiji kadhaa kwenye jimbo la Enga pia viliathirika baada ya sehemu ya mlima kuanguka mapema jana Ijumaa.

Karibu watu 300 wanahofiwa kufunikwa na matope, hii ikiwa ni kulingana na baadhi ya vyombo vya habari vikinukuu taarifa za mamlaka za eneo hilo.

Kulingana na vyombo hivyo, zaidi ya watu 3,000 wanaishi kwenye eneo hilo lililoathirika.