Mamia washiriki maandamano ya ″Komesha Ebola″ Congo | Matukio ya Afrika | DW | 23.08.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mamia washiriki maandamano ya "Komesha Ebola" Congo

Mamia ya watu walikusanyika mjini Goma kuonyesha mshikamano wa wahudumu wanaopambana na Ebola ambao wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara katika maeneo ambako Ebola inaendelea kusambaa.

Gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini Carly Kasivita, alieandaa mandamano hayo alisema yeyote anaesambaza taarifa za upotoshaji na kuda kuwa "Ebola ni biashara" atakamatwa.

"Tuna wasiwasi mkubwa .... Baadhi ya wachungaji, baadhi ya wanasiasa, wanajiingiza kwenye mjadala  kuhusu afya ya umma na kuwapotosha wengi wa raia wetu kwa taarifa zisizo na ukweli. Wachungaji hawa wanaokanusha uwepo wa Ebola wataswekwa jela mara watakapokamatwa," alisema Kasivita.

Gavana huyo pia aliahidi maandamano zaidi na mikakati ya kuongeza ufahamu katika maeneo mengine ya mkoa, yakiwemo beni na Butembo amabko Ebola imeenea pia.

"Ujumbe ni kusema laazima tukomeshe maradhi haya katika mkoa. Katika namna tulivyo na wasiwasi kuhusu usalama mkaoni, ndivyo tulivyo kuhusu Ebola," alisema.

Demokratische Republik Kongo l anhaltende Ebola-Epidemie (Reuters/O. Acland)

Mfanyakazi w afya akitoa chanjo ya Ebola katika kituo cha afya cha Himbi mjini Goma.

Watu waliendesha baiskeli sambamba na polisi, wanajeshi na wakaazi mjini Goma wakiwa wamebeba mabango na kuvalia Fulana zenye ujumbe unsema "KOMESHA".

"Hatutaki mataifa mengine yaambukizwe kupitia mkoa wetu mzuri wa Kivu Kaskazini. Tunataka kila mmoja achangia kukomesha Ebola," Kasivita alisema. " Watu wanahitaji kuelewa kwamba ugonjwa huu upo na tunawatolea mwito makundi ya waasi kushirikiana na timu za uitikiaji kwa sababu kuna mazingira ambako timu hizo haziwezi kufika kwa sababu za kiusalama."

Hakuna dalili za kupungua makali

Mripuko wa Ebola, ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,800 tangu ulipotangazwa mwaka mmoja uliopita mashariki mwa Congo, haujaonyesha dalili za kupungua licha ya tiba mpya na chanjo zilizotolewa kwa zaidi ya watu 197,000 katika eneo hilo.

Visa vipya vilizuka mjini Goma, ambao ndiyo mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, katika miezi y akaribuni na ugonjwa huo umesambaa katika mkoa mpya katika muda wa wiki iliyopita.

Der Direktor des National Institute of Biomedical Research (INRB), Jean-Jacques Muyembe (AFP/Getty Images/M. Alexandre)

Mkuu wa huduma ya kupambana na Ebola nchini Congo, Jean-Jacques Muyembe.

Ukosefu wa usalama umekuwa suala moja katika eneo ambako makundi ya waasi yamepigania udhibiti wa maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini kwa miongo kadhaa. Ebola imeenea kwa sababu ya ukosefu wa imani miongoni mwa jamii zinazopanga mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa afya.

Gavaba wa mkoa wa Kivu Kusini na mwezake wa Rwanda katika mkoa wa Magharibi walisaini makubaliano ya pande mbili siku ya Jumatano mjini Bukavu, kuunganisha juhudi zao katika mapambano dhidi ya Ebola, huku wakiheshimu haki za watu kuvuka mipaka.

Ili kusaidia kuzuwia kuenea zaidi kwa Ebola, hata hivyo, ujumbe wa pande hizo mbili ulikubaliana kubadilishana taarifa, ikiwemo orodha ya watu wenye hatari kubwa, alisema Daniel Lwaboshi, naibu mkuu wa utumishi wa gavana wa Kivu Kusini.

"Hawa ni watu ambao wamekaribiana na wagonjwa kwa sababu tunao kwenye mkoa wetu," alisema. Hatua zimechukuliwa tayari. Siku kadhaa zilizopita, watu kadhaa kutoka Kivu Kusini walikuwa wamezuwiwa kuvuka mpaka.

Chanzo:ape