1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Hamas na Houthi wajadili kutanua makabiliano na Israel

16 Machi 2024

Maafisa kutoka makundi mbalimbali ya mamlaka ya Palestina wakiwemo wanamgambo wa Hamas, walikutana siku chache zilizopita na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran ili kuratibu shughuli zao.

https://p.dw.com/p/4dnvY
Kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh
Kiongozi wa kundi la Hamas Ismail HaniyehPicha: Marwan Naamani/dpa/picture alliance

Shirika la habari linaloiunga mkono Iran Al Mayadeen, limeripoti kuwa maafisa wakuu wa Hamas, wanamgambo wa Islamic Jihad na kundi linalopigania ukombozi wa Palestina walihakikishwa na Wahouthi kwamba wataendelea na hujuma katika bahari ya Sham licha ya mashambulizi ya anga ya Marekani na Uingereza.

Mkutano huo, ambao ukumbi wake haukuwekwa wazi, ulikuwa sehemu ya kujiandaa kwa uwezekano wa kuongezeka kwa mzozo na mashambulizi zaidi ya Israel katika mji wa Rafah ambapo zaidi ya Wapalestina milioni moja wamekimbilia kutafuta hifadhi.

Soma pia: Malori ya misaada ya WFP yawasili Gaza

Waasi wa Houthi wamekuwa wakizishambulia meli katika bahari ya Sham na ghuba ya Aden katika kile wanachosema ni kuonyesha mshikamano kwa Wapalestina.

Hata hivyo, hakukuwepo na kauli yoyote kutoka makundi hayo manne kuhusu mkutano huo.