1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroColombia

Makundi haramu yenye silaha Colombia yalijiimarisha 2023

7 Mei 2024

Ripoti ya siri iliyotolewa na mamlaka za usalama nchini Colombia imebainisha kuwa vikundi vinne vikuu vyenye silaha nchini humo vilijiimarisha mnamo mwaka 2023.

https://p.dw.com/p/4faym
Waasi wa ELN
Waasi wa ELN ni mojawapo ya makundi kongwe zaidi ya waasi katika bara la Amerika Kusini Picha: Raul Arboleda/AFP/Getty Images

Ripoti ya siri iliyotolewa na mamlaka za usalama nchini Colombia imebainisha kuwa vikundi vinne vikuu vyenye silaha nchini humo vilijiimarisha mnamo mwaka 2023 na kuongeza udhibiti wa maeneo wanayoyashikilia kutokana na biashara haramu ya madawa ya kulevya na uchimbaji haramu wa madini ya dhahabu.

Soma pia: Kundi la waasi Colombia latangaza kuanza tena utekaji nyara

Ripoti hiyo ililenga kundi la wapiganaji wa mrengo wa kushoto linalojiita Jeshi la Kitaifa la Ukombozi (ELN), genge la wahalifu la "Clan del Golfo" na pande mbili hasimu za kundi la waasi wa FARC ambao sasa wameweka silaha chini, kundi la Estado Mayor Central (EMC) na Segunda Marquetalia.

Soma pia: Mazungumzo ya amani yasambaratika Colombia

Rais wa mrengo wa kushoto wa Colombia, Gustavo Petro ameahidi kuvimalizika vita vilivyodumu miaka 60 na ambavyo vimesababisha vifo vya watu wasiopungua 450,000. Rais Petro ameahidi kuvimaliza vita hivyo ama kwa njia ya amani au kwa wahusika kujisalimisha, lakini imekuwa vigumu kufikia makuabliano na makundi yote.