Majeshi yakabidhi silaha. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Majeshi yakabidhi silaha.

Abdijan. Majeshi ya serikali na yale ya waasi wa zamani nchini Ivory Coast wameanza hatua za kukabidhi silaha ikiwa ni hatua muhimu katika kupatikana amani ya kudumu tangu pale yaliyotokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe miaka mitano iliyopita.

Zimefanyika sherehe siku ya Jumamosi katika miji katika pande zote ambapo nchi hiyo imegawika baina ya eneo linalotawaliwa na waasi upande wa kaskazini na lile la upande wa kusini linalodhibitiwa na serikali tangu mwaka 2003.

Rais Laurent Gbagbo pamoja na waziri mkuu wake , kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro, walihudhuria sherehe hiyo katika mji wa kati wa soko wa Tiebissou. Makubaliano ya amani ya mwezi March kati ya serikali ya rais Gbagbo na majeshi ya waasi wanaoongozwa na Soro yaliweka msingi kwa ajili ya hatua za kurejesha silaha. Makubaliano hayo pia yanatoa wito wa kufanyika uchaguzi ifikapo katikati ya mwaka ujao.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com