Mahakama Zimbabwe yamkuta mwanaharakati bila hatia | Matukio ya Afrika | DW | 29.11.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Mahakama Zimbabwe yamkuta mwanaharakati bila hatia

Mahakama ya Zimbabwe imemfutia mashtaka ya uasi mchungaji Evan Mawarire baada ya kumkuta hana hatia

Mahakama ya Zimbabwe imemfutia mashtaka ya uasi mchungaji Evan Mawarire baada ya kumkuta hana hatia. Mawarire ambaye pia ni mwanaharakati, alifunguliwa mashtaka hayo na utawala uliopita wa Robert Mugabe.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe, Priscilla Chigumba ametoa uamuzi huo leo, akisema upande wa serikali haukutoa ushahidi dhidi ya kesi ya mchungaji huyo.

Mawarire amesema amefurahishwa na uamuzi huo na kwamba kipindi chote cha kesi hiyo kilikuwa cha ajabu na hakupaswa kukamatwa.

Amemtaka rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa kuheshimu haki za binaadamu, akisema watu wataandamana tena iwapo wataona serikali mpya inakiuka uhuru wao. Mawarire alikuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Mugabe.