1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya kimataifa ICC yamhukumu Bemba

Zainab Aziz
18 Septemba 2018

Mahakama ya ICC imempiga faini Jean-Pierre Bemba dola laki tatu kwa kosa la kuvuruga ushahidi na kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja gerezani

https://p.dw.com/p/351AT
DR Kongo Jean-Pierre Bemba
Picha: Getty Images/AFP/P. Mulongo

Mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague, ICC, imemhukumu mwanasiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jean-Pierre Bemba faini ya dola laki tatu na kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kuvuruga ushahidi.

Hata hivyo, Bemba hatakwenda jela kutokana na muda ambao ameshautumikia kifungoni hapo awali. Mwanasiasa huyo alifutiwa mashtaka ya kutenda uhalifu wa kivita baada ya kukata rufani mnamo mwezi wa Juni, lakini alihukumiwa kwa mashtaka ya uzito wa chini ya kuvuruga ushahidi.

Hukumu hii ya leo inazizima kabisa jitihada za Bemba kugombea katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mnamo mwezi Desemba katika Jamhuri ya Kidemokrasia  ya Kongo, ambao tangu hapo alishazuiliwa na Tume ya Uchaguzi na Mahakama ya Katiba ya nchi yake.