Mahakama ya Juu Kenya yaamuru uchaguzi mpya wa rais | Matukio ya Afrika | DW | 01.09.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Mahakama ya Juu Kenya yaamuru uchaguzi mpya wa rais

Mahakama ya Juu nchini Kenya imeamuru kurejewa kwa uchaguzi wa rais nchini humo, ikiyafuta yale ya awali yaliyokuwa yamempa ushindi Rais Uhuru Kenyatta. 

Mahakama hiyo imesema kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu kwenye uchaguzi wa tarehe 8 Agosti kiasi cha kuvunja hata katiba ya taifa hilo la Afrika Mashariki. 

Uchaguzi mpya umeamuriwa kufanyika ndani ya siku 60 kutoka sasa. 

Mgombea wa upinzani, Raila Odinga, alikuwa amedai kuwa matokeo ya kura kwa njia ya elektroniki yalidukuliwa na kuchakachuliwa kumsaidia Uhuru Kenyatta wa chama tawala, Jubilee. 

Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, ilikuwa imemtangaza Kenyatta mshindi wa asilimia 54 ya kura.

Wakeya kadhaa waliamua kuingia mitaani kupinga matoeo hayo na walikuwa wamedhamiria kuingia tena endapo mahakama ingelipitisha ushindi huu. 

Hii ni mara ya pili kwa Odinga kupinga matokeo mahakamani, lakini mwaka 2013 alishindwa.

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com