Waandamanaji nchini Iran wakabiliwa na adhabu ya kifo
14 Januari 2026
Mkuu huyo wa Mahakama pia amesema uendeshwaji huo wa haraka, utahusisha pia hukumu za kifo.
Jaji Mkuu wa Iran Gholamhossein Mohseni-Ejei ametoa matamshi hayo katika video iliyosambazwa na televisheni ya taifa ya Iran mtandaoni, wakati wanaharakati wakitahadharisha kwamba watuhumiwa huenda wakanyongwa hivi karibuni.
"Kama mtu alimchoma mtu, akamkata kichwa na kumchoma moto basi ni lazima tufanye kazi yetu haraka," alisema Jaji Mohseni-Ejei.
Maoni yake yanachukuliwa kama ukaidi wa moja kwa moja dhidi ya Trump, ambaye siku ya Jumanne aliionya Iran kuhusu kuwanyonga watu katika mahojiano na kituo cha CBS.
Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Binadamu lenye makao yake Marekani liliripoti kuwa karibu watu 2,571 wameuawa kufuatia hatua kali dhidi ya waandamanaji