1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Kuimarishwa kwa sheria ya waomba hifadhi

Sekione Kitojo
3 Januari 2019

Magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha na uhalifu uliotokea mjini Amberg na Bottrop, ambako wageni wanaoomba hifadhi waliwashambulia watu mjini Amberg na pia katika mji wa Essen, Mjerumani alishambulia raia wa kigeni.

https://p.dw.com/p/3Axve
Deutschland Mann fährt in Fußgängergruppe
Picha: picture-alliance/dpa/M. Kusch

Mhariri  wa  gazeti  la  Der neue Tag  akiandika  kuhusu  uhalifu  huo mjini  Amberg  na  Bottrop  anasema  kwamba  ni  hatari na  makosa , kwamba mashambulizi  yaliyotokea  mjini  Amberg  yanachukuliwa kisiasa  zaidi, wakati  mtu  ambaye ameonesha  chuki  dhidi  ya wageni  katika  eneo  la  Essen  kuwa  ni mtu  aliyechukua  uamuzi wa  pekee  na  mwenye  matatizo  ya  akili. Kile  matukio yote  mawili yanachoshabihiana, ni  kwamba   matukio  hayo  yamefanywa  na wanaume  kwa  matumizi  ya  nguvu.

Kila  mara  ni  wanaume. Kwa  hiyo  kuna  maswali  mengi  muhimu. Vipi  jumuiya ya  watu  wapenda  amani  wanaweza  kudhibiti  hali  hii ya watu  kutaka  kufanya  uhalifu  huu?

Nae  mhariri  wa  gazeti  la Berliner Morgenpost akizungumzia  mada hiyo  anaandika: Waziri  wa  mambo  ya  ndani  Horst Seehofer amechukua  uamuzi  mkali  dhidi  ya  kundi  la  vijana  wanne wanaaomba  hifadhi  ambao  walipigana. Lakini  baada  ya  tukio la wafuasi wa  siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia  mjini  Chemnitz Seehofer  alitumia  zaidi  ya  wiki  moja. Lilipotokea  tukio  la  Amberg lakini  alitumia  siku  tatu.  Anatakiwa  pia  kuweka  sawa  tukio  la shambulio  la  mjini  Bottrop.

Tukio  hilo  lilifanywa  na  Mjerumani  kutokana  na  chuki  dhidi  ya wageni, na  kuwagonga  watu  kwa  gari  yake akiwalenga  watu wenye  asili  ya  kigeni. Matukio  yote  mawili  yanaonesha  upana wa ghasia  zinazohusiana  na  matokeo  ya  mzozo  wa  wakimbizi wa  mwaka  2015. Kile  kilicho  muhimu  zaidi ni  utulivu  wa  kisiasa na  kuchukua  hatua  za  usawa na  haki. Badala  ya  kupiga  kelele na  kuwa  mfano  wa  chama  cha  AfD, Seehofer  na  chama  cha CSU wanapaswa kuisaidia  nchi  kufikia  malengo  sahihi.

Gazeti  la  Stuttgarter Zeitung, linazungumzia  kuhusu miaka  20  ya sarafu  ya  euro  katika  mataifa  ya  Umoja  wa  Ulaya. Umoja  wa sarafu  bila  kuwa  na  umoja  wa  kisiasa  hauwezekani, wamewahi kuonya  wakosoaji wa  sarafu  hiyo. Hali  ya  kutowezekana  haipo, kama  ilivyoonekana  katika  miaka  20  iliyopita, lakini  kuna  ugumu.

Wanasiasa  katika  mataifa  ya  Ulaya  wanajiuliza  maswali  mengi na  hawajapata muafaka  kuhusiana  na  lengo  lao, iwapo  kutatokea mzozo  mkubwa.

Mzozo  wa  dunia  wa  fedha  na  biashara  pamoja  na  hali  ya  wasi wasi  mkubwa  ndani  ya  kanda  ya  sarafu  ya  euro ni  matokeo  ya hilo. Benki  kuu  wa  Ulaya  inajitokeza  tu  kama  jeshi  la  zima moto.

Nae  mhariri  wa  gazeti  la  Emder  Zeitung akizungumzia  kuhusu sarafu  hiyo  ya  euro limeandika:  Wengi  wa  Wajerumani wanataka  pia katika  enzi  hizi  za  kidigitali  kutoachana  na  sarafu na  noti. Hili  bila  shaka  linafahamika. Kwa  hiyo  huo  ni uwezekano  tu  wa kudhibiti, hali  ya  kuingia  kikamilifu  katika utaratibu  wa  malipo  kwa  njia  za  kielektroniki unapaswa kufanyiwa tafakuri.

Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Idd Ssessanga