Madagascar wapepea, Algeria kazi rahisi AFCON | Michezo | DW | 08.07.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Madagascar wapepea, Algeria kazi rahisi AFCON

Madagascar Jumapili waliwafunga Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo magoli 4-2 kupitia mikwaji ya penalti na kujikatia tiketi ya robo fainali ya Kombe la Mataifa Barani Afrika.

Beki wa Congo Chancel Mbemba alifunga goli la kusawazisha na kufanya mambo kuwa sawa magoli 2-2 na kupelekea mikwaju ya penalti kupigwa baada ya mambo kuwa sawa katika muda wa ziada.

Algeria nao waliendelea kuthibitisha kwamba ni mojawapo ya timu zinazopigiwa upatu kulinyakua kombe hilo la ubingwa wa Afrika kwa kupata ushindi wa rahisi wa 3-0 walipokuwa wakipambana na Guinea kwenye mechi yao ya raundi ya timu kumi na sita bora.

Siku ya Jumatatu ni zamu ya Mali kuzipiga na Ivory Coast kisha Ghana na Tunisia watatunishiana misuli katika mechi ya pili.