1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron afanya mkutano na Mwanamfalme bin Salman mjini Paris

16 Juni 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo amekuwa mwenyeji wa Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ambapo wamefanya mazungumzo mjini Paris.

https://p.dw.com/p/4ShCT
Rais Emmanuel Macron na mgeni wake Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia
Rais Emmanuel Macron akiwa na mgeni wake Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia mjini ParisPicha: Abd Rabbo Ammar/ABACA/picture alliance

Madhumuni ya Macron kufanya mkutano huo ilikuwa ni kujaribu kumrai kiongozi huyo wa nchi hiyo ya kifalme yenye utajiri wa mafuta kutoa matamshi ya kuiunga mkono Ukraine katika mzozo wake na Urusi.

Macron pia anatarajiwa kujadili na Mwanamfalme huyo juhudi za kupata suluhu katika hatua za kumtafuta rais mpya wa Lebanon, mkwamo ambao unazidi kuipa wasiwasi Ufaransa.

Ziara ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 37 inakuja chini ya mwaka mmoja baada ya ziara yake ya mwisho huko Paris na inaonyesha mahusiano mazuri yaliyoko kati ya Ufaransa na Saudi Arabia.

Ziara hiyo imewaghadhabisha wanaharakati kufuatia mauaji ya mwandishi na mkosoaji wa utawala wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Saudia nchini Uturuki.