1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maambukizi ya Ebola yaenea kwa kasi mashariki mwa DRC

22 Mei 2026

Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kimeendelea kupanda kwa kasi, kwa mujibu wa mamlaka za maeneo hayo.

https://p.dw.com/p/5EAvo
DR Congo Rwampara 2026 | Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu katika kituo kutibu Ebola
Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakikusanyika kuua vijidudu katika hospitali kuu ya Rwampara kabla ya kushughulikia mwili wa mtu aliyefariki kutokana na Ebola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Gradel Muyisa Mumbere/REUTERS

Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kimeendelea kupanda kwa kasi, kwa mujibu wa mamlaka za maeneo hayo. Wizara ya afya nchini humo imeripoti visa 671 vya maambukizi na kiasi cha vifo 160 vinavyohusishwa na ugonjwa huo. Kulingana na wizara hiyo, visa 64 vya maambukizi na vifo 6 vimethibitishwa kupitia vipimo vya maabara.

Wakati huo huo, watu kadhaa walichoma moto kituo cha matibabu ya Ebola katika mji wa Rwampara ulioko mashariki mwa Congo jana, baada ya kuzuiwa kuchukua mwili wa mwanaume mmoja wa eneo hilo.

Ugonjwa huo umekuwa ukisambaa kwa wiki kadhaa katika eneo lisilo na miundombinu ya kutosha ya afya na ambako watu wengi bado wanakimbia migogoro ya makundi yenye silaha.”