Lusaka: Muingereza aamriwa kuihama zambia | Habari za Ulimwengu | DW | 20.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Lusaka: Muingereza aamriwa kuihama zambia

Serikali ya Zambia imemuondoa nchini raia mmoja wa Uingereza kwa madai ya kumkashifu Rais Levy Mwanawasa na kutumia lugha ya matusi dhidi ya wafanyakazi wake. Msemaji wa wizara ya uhamiaji Mulako Mbangweta alisema Smart Edward mwenye umri wa miaka 44 alitakiwa kuihama Zambia jana, kwa sababu kuweko kwake kunaweza kuhatarisha amani na utulivu. Hata hivyo alikataa kuelezea ni maneno gani aliyoyatumia kumakashifu rais Mwanawasa. Edwards alikua ni meneja wa kanda wa mradi wa ushauri na mafunzo nchini Zambia. Alisafirishwa kwa ndege hadi Afrika kusini akiwa njiani kurudi London.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com