London. Anayetuhumiwa kumuua Litvinenko atakiwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 29.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

London. Anayetuhumiwa kumuua Litvinenko atakiwa.

Uingereza imeiomba rasmi Russia kumpeleka nchini humo mtu anayetuhumiwa kuumuua wakala wa zamani wa Ujasusi wa Russia Alexander Litvinenko.

Maafisa wamethibitisha kuwa balozi wa Uingereza ametoa ombi hilo la kupelekwa kwa Andrei Lugovoi kwa wizara ya mambo ya kigeni ya Russia.

Waendesha mashtaka wa Uingereza wamesema wiki iliyopita kuwa wanataka kumfikisha Lugovoi mbele ya mahakama ya Uingereza na kumshtaki kwa kumpa sumu Litvinenko mjini London Novemba mwaka jana.

Lugovoi amekuwa akikanusha kuhusika katika mauaji ya Litvinenko.

Sheria za Russia zinazuwia kupelekwa raia wake nje ya nchi hiyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com