1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLithuania

Lithuania yatangaza dharura kutokana na maputo ya Belarus

9 Desemba 2025

Serikali ya Lithuania imetangaza hali ya dharura ya kitaifa kutokana na hatari za kiusalama zinazosababishwa na maputo ya Belarus, mshirika wa Urusi ambayo yamekiuka anga ya Lithuania katika wiki za hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/550Iq
Lithuania 2025 | Usafirishaji wa sigara kwa puto kutoka Belarus hadi mpaka wa Umoja wa Ulaya
Afisa akikagua puto linalotumika kubeba sigara hadi Lithuania, kwa sababu wasafirishaji haramu wa Belarus mara nyingi hutumia kusafirisha bidhaa haramu hadi Umoja wa UlayaPicha: Uncredited/AP Photo/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Lithuania, Vladislavas Kondratovicius ameliambia Baraza la Mawaziri kwamba hali hiyo ya dharura imetangazwa kutokana na usumbufu wa usafiri wa anga na wasiwasi wa usalama wa taifa.

Mvutano kati ya Lithuania na Belarus umeongezeka baada ya maputo ya hali ya hewa kutoka Belarus kuilazimisha Lithuania kufunga uwanja wake mkuu wa ndege mara kadhaa wiki zilizopita na kukwamisha  maelfu ya watu.

Ingawa maputo hayo hutumiwa kuingiza biashara haramu ya sigara nchini Lithuania, maafisa wa Vilnius wanachukulia kama vitendo vya makusudi vya usumbufu vinavyopangwa na Belarus.