1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ligi ya Ujerumani Bundesliga kuanza  mwishoni mwa juma

Sekione Kitojo
14 Septemba 2020

Ligi ya Ujerumani kuanza kurindima mwishoni mwa juma , Bayern ikipambana na Schalke 04

https://p.dw.com/p/3iSfE
Fußball Robert Lewandwoski
Picha: picture-alliance/SvenSimon/F. Hoermann

Ligi ya Ujerumani inarejea uwanjani mwishoni mwa juma hili, mchezo wa ufunguzi ukiwa siku  ya  Ijumaa tarehe 18.09 kati ya mabingwa watetezi Bayern Munich wakiikaribisha  Schalke 04  mara hii.

Fußball Borussia Dortmund | Erling Haaland
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling HaalandPicha: picture-alliance/SvenSimon/E. Kremser

Lakini kabla  ya  kufunguliwa  msimu  wa  ligi , kuanzia  siku  ya  Ijumaa kumekuwa  na  michezo  ya  duru  ya  kwanza  ya  kombe  la shirikisho DFB Pokal  hapa  Ujerumani, ambapo  hadi jana  timu pekee  ya  daraja  la  kwanza  iliyoyaaga  mashindano  hayo  ni Hertha BSC  baada  ya  kutandikwa  mabao 5-4 na Braunschweig.

Leo hii jioni ni  zamu ya bingwa mtetezi Bayern Munich wakipambana na  timu  ya  daraja la  4 Dueren, Borussia  Dortmund  itaoneshana kazi na timu  ya  daraja  la  tatu  ya  MSV Duisburg. Wakati Rot Weis Essen itakuwa  mwenyeji  wa  Arminia  Bielefeld, Hannover itakwaana  na  Wuezburger Kickers na  Hamburg Sport Verein ina miadi  na  Dynamo Dresden.

Deutschland Symbolbild 1. FC Köln
Mashabiki bado hawataruhusiwa kuingia uwanjani hadi baada ya mwezi OktobaPicha: Imago Images/Kirchner-Media/Neundorf

Serikali kuu  ya  Ujerumani  inaendelea na mtazamo wa uwiano wa nchi nzima kuhusiana na  sheria wakati linakuja suala la  kurejea kwa mashabiki katika  viwanja  vya michezo. Msemaji wa  serikali Steffen Seibert alirudia leo azimio lililotolewa  mwezi Agosti na kansela Angela  Merkel na mawaziri wakuu  wa  majimbo nchini Ujerumani. Ilikubalika kuwa kikosi  kazi kitateuliwa  kuwasilisha mapendekezo na ushauri  hadi mwishoni mwa Oktoba. Maelekezo ya  mawaziri wakuu na kansela  kwa kikosi kazi hicho bado yanatumika, alisema  Seibert.

Ligi ya  Ujerumani itaanza  rasmi hapo Ijumaa  tarehe 18, kati ya Bayern Munich  na Schalke 04, mashabiki na  wachambuzi wanatarajia  nini  katika  msimu  huu  wa 57 wa Bundesliga.