Lewis Hamilton aendelea kutawala Formula One | Michezo | DW | 12.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Lewis Hamilton aendelea kutawala Formula One

Inadhihirika wazi kuwa mashindano ya magari ya Formula One yanatumbuizwa na timu moja ambayo inaendelea kuutawala msimu huu. Hii ni baada ya timu ya Mercedes kunyakua ushindi katika mbio za Uhispania

Kiongozi wa timu ya Red Bull Christian Horner alidokeza kuhusu uwezekano wa timu ya Mercedes kushinda mikondo yote 19 ya msimu huu, baada ya dereva Lewis Hamilton kushinda mbio za Barcelona jana mbele ya mwenzake Nico Rosberg. Madereva wa Red Bull Daniel Ricciardo na Sebastian Vettel walimaliza katika nafasi za tatu na nne mfululizo, lakini kwa pengo kubwa.

Timu ya Mercedes imejikusanyia pointi 197 katika mbio tano za kwanza msimu huu, na ushindi wa Hamilton ulikuwa wake wa nne mfululizo. Macho sasa yataelekezwa mjini Monaco, Ufaransa wikendi ijayo, na Rosberg anafahamu kuwa amemkaribia sana Hamiltion, lakini itategemea na ni nani atakayeshika nafasi za kwanza wakati wa mazoezi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-rahman