Leverkusen yampata kocha mpya | Michezo | DW | 06.03.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Leverkusen yampata kocha mpya

Bayer Leverkusen wamemtangaza Tayfun Korkut kuwa kocha wao mpya. Kocha huyo wa zamani wa timu za Hannover na Kaiserslautern amepewa mkataba wa hadi ya mwisho wa msimu huu

Leverkusen ilinyesheshwa mvua ya mabao 6-2 na Borussia Dortmund. Leverkusen hawakuchelewa kumtimua Schmidt ambaye kwa muda mrefu amekuwa chini ya shinikizo

Korkut amekaribishwa leo rasmi uwanjani BayArena ikiwa ni chini ya saa 24 baada ya kumpiga kalamu Roger Schmidt. Korkut mwenye umri wa miaka 42, ana ujuzi wa Bundesliga.

Mpango wa Leverkusen ni kuukamilisha msimu huu chini ya ukufunzi wa Korkut, kabla ya kuingia sokoni na kumleta mtu wanayemwona anaweza kufanya kazi kwa kipindi kirefu. Miongoni mwa majina yaliyojitokeza katika uvumi wa vyombo vya habari ni Julian Nagelsmann wa Hoffenheim na Lucien Favre wa Nice.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu