Leon Goretzka asema atahamia Bayern | Michezo | DW | 19.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Leon Goretzka asema atahamia Bayern

Mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Leon Goretzka anatarajiwa kuhamia katika klabu ya Bayern Munich.

Leon Goretzka ameiarifu klabu yake ya Schalke 04 kuwa hataurefusha mkataba wake wa sasa unaomalizika mwishoni mwa msimu huu. Mkurugenzi  wa  spoti  wa Schalke Christian Heidel amesema  katika  ukurasa  wa  Twitter Ijumaa kwamba "ametuarifu mwanzoni  mwa  wiki  hii  kwamba  ana nia ya  kuihama  klabu hiyo  na  kujiunga  na  Bayern Munich,"

Bayern  hawajathibitisha  hatua  hiyo  ya  kuhama  lakini  kwa  mujibu wa  Heidel  mchezaji huyo  amesaini mkataba  wa  kuanzia  Juni  mosi, baada  ya  mkatba  wake  wa  sasa  na Schalke kufikia  mwisho.

Fußball FC Schalke 04 v 1. FSV Mainz 05 - 1. Bundesliga Torjubel 1:0 (Imago/Team 2)

Leon Goretzka atakuwa na Schalke 04 hadi mwishoni mwa msimu huu 2017/18 tu

Goretzka  mwenye  umri  wa  miaka  22 , alijiunga  na  Schalke  akitokea  Bochum mwaka 2013 na  amekuwa  mchezaji wa timu ya kwanza  na timu hiyo pamoja  na  timu  ya  taifa, akishinda  taji  la  mabara  Confed Cup  mwaka  2017  nchini  Urusi  na  kufunga  mabao 6 katika  michezo 12  aliyoitumikia  timu  ya  taifa.

Mwandishi_: Sekione Kitojo / dpae