1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leclerc ashinda mbio za ufunguzi wa msimu Bahrain Grand Prix

Bruce Amani
21 Machi 2022

Charles Leclerc wa timu ya Ferrari alishinda mbio za ufunguzi wa msimu za Bahrain Grand Prix Jumapili baada ya bingwa mtetezi Max Verstappen kujiondoa kutokana na tatizo la umeme na ikiwa imesalia mizunguko miwili.

https://p.dw.com/p/48nIU
Charles Leclerc
Picha: Hassan Ammar/AP/picture alliance

Katika mashindano ya mbio za magari ya Formula One Charles Leclerc wa timu ya Ferrari alishinda mbio za ufunguzi wa msimu za Bahrain Grand Prix Jumapili baada ya bingwa mtetezi Max Verstappen kujiondoa kutokana na tatizo la umeme na ikiwa imesalia mizunguko miwili.

Leclerc alielezea furaha yake baada ya ushindi huo. "Inapendeza, inapendeza sanaa. Baada ya kazi ngumu ya kufuzu jana ili kuanza katika nafasi ya kwanza, inafurahisha saana lakini ilibidi nimalizie kazi hiyo leo na kwa kumaliza katika nafasi mbili za kwanza kwa timu ni kitu kizuri mno na haikuwa kazi rahisi." Alisema Leclerc.

Carlos Sainz wa Ferrari alimaliza katika nafasi ya pili huku Sergio Perez akikamilisha siku ya majanga kwa timu ya Verstappen ya Red Bull kwa kujiondoa baada ya gari lake kuzima kwenye mzunguko wa mwisho kutokana na tatizo la kiufundi. "Nadhani mwishowe tatizo kubwa ni kuwa hatukupata pointi hata moja licha ya ubora wa gari letu na bila shaka katika siku ambazo unakumbwa na matatizo madogo madogo au haujafurahishwa kabisa na usawa ulio nao ili kupambana na kupata pointi na tulichokifanya leo bila shaka inaumiza sana." Anasema Max.

Hiyo ilimpa fursa Lewis Hamilton wa Mercedes kumaliza katika nafasi ya tatu. George Russell, katika mbio zake za kwanza tangu alijiunga na Hamilton akiichukua nafasi ya Valtteri Bottas, alimaliza wan ne na kuwapa Mercedes pointi 27 ambayo wasingetarajia kuzipata kabla ya kuanza mbio hizo.

Kutakuwa na mapunziko mafupi kabla ya madereva kuelekea Saudi Arabia kwa mbio za wikiendi ijayo.

  afp