Kupitisha maamuzi binafsi – Kupanga uzazi | Noa Bongo | DW | 01.03.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Noa Bongo

Kupitisha maamuzi binafsi – Kupanga uzazi

Idadi ya watu barani Afrika inazidi kuongezeka. Familia zinazidi kupanuka huku raslimali zikizidi kuwa haba, hali inayotoa taswira ya hali ngumu ya maisha.

Kuna haja ya kufahamu jukumu tunalopasa kutekeleza katika mpango wa uzazi

Kuna haja ya kufahamu jukumu tunalopasa kutekeleza katika mpango wa uzazi

Sababu kubwa inayochangia kuongezeka haraka kwa idadi ya watu duniani ni ukosefu wa habari muhimu. Katika mfululizo wa vipindi hivi tunajifunza njia za kuepukana na mimba zisizotarajiwa au kupangiwa, na pia jinsi ya kujiepusha na gonjwa la ukimwi au magonjwa mengine yanayosababishwa na kufanya mapenzi. Vipindi hivi pia vinakupa habari za kimsingi kuhusu njia unazoweza kutumia kupanga uzazi.

Desirée mwenye umri wa miaka 16, ndiye kinara katika mchezo huu wa redio. Baaada ya mamake kufariki, anachukua jukumu la kuwalea watoto wengine watano huku akiendelea na juhudi za kupata elimu bora. Hali kadhalika Desirée anajaribu kukabiliana na mawazo ya bibi yake yaliyopitwa na wakati kuhusu suala na jukumu la mwanamke katika jamii.

Mambo yanazidi kubadilika wakati msichana huyu anapokutana na Eric, mvulana wa umri wa miaka 18 na ambaye anataka mengi zaidi ya urafiki wa kawaida. Na kisha Desirée anakuja kufahamu siri anayotumia Lorraine, rafiki yake wa dhati.

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘ Noa bongo Jenga Maisha yako’ vinasikika katika lugha sita; Kingereza, Kifaransa, Kiswahili, Hausa, Kireno na Amharic. Na vinafadhiliwa na wizara ya nchi za kigeni ya Ujerumani.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa