Kufunguliwa kwa gaidi Christian Klar | Magazetini | DW | 25.11.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Kufunguliwa kwa gaidi Christian Klar

Ndio mada kuu iliohaririwa na magazeti ya leo.

Angela Merkel na Nicolas Sarkozy.

Angela Merkel na Nicolas Sarkozy.

Safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo, zimetuwama zaidi juu ya uamuzi wa Mahkama kumtoa gerezani gaidi maarufu wa Jeshi Jekundu la Ujerumani la Baader-Meinhof -RAF-Christian Klar.Wahariri wamechambua pia kikao cha pamoja cha baraza la mawaziri baina ya Ujerumani na Ufaransa kilichofanyika jana mjini Paris. Gazeti la Volkstimme kutoka Magdeburg juu ya kikao hicho,Laandika:

"Ikiwa Kanzela Angela Merkel na rais Nicholas Sarkozy, hawana chochote muhimu cha kutangaza,hujaribu kutoa dhana kana kwamba wnacho.Mara hii ni msukosuko mkubwa wa fedha unaozidi kutapakaa. Kanzela Merkel ameungama binafsi kwamba kila siku,kila saa,makisio ya hali ya uchumi itakavyokua hubadlika huku serikali zikijikuta zinatunga mpango wao wa kwanza wa kukabiliana na msukosuko huo.

Hivyo ni kuungama kwamba wanasiasa hawana uwezi wa kupambana na msukosuko huu wa uchumi uliozuka .Waweza tu kupambana na athari zake tu n a kuzipunguza."

Volksstimme linaonya kuwa yule leo anaeamini kwa kupunguza kila nchi kodi za mapato ataweza kuutia jeki uchumi ,huyo hakutambua msukosuko huu ulioikumba dunia nzima ,mipango ya kitaifa yaweza haraka kuzifilisi fedha.

Ama likituchukua katika mada kuu ya wahariri wa magazeti ya leo-kufunguliwa kutoka korokoroni kwa gaidi wa RAF (Jeshi Jekundu la Ujerumani) Christian Klar, gazeti la Nordwest-Zeitung laandika:

"Hakuna jina la gaidi mwengine mbali na Baader na mwenzake Meinhof linalofungamanishwa mno na ugaidi wa RAF kama la Christian Klar.Kwa bahati mbaya ,kuna uwezekano sasa akaalikwa katika mazungumzo ya vyombo vya habari ambamo hata akalipwa ujira na kuongeza uchungu na maudhi kwa jamaa wa waliouwawa.Ingelikuwa uzuri pia kwa vyombo vyetu vya dola kwa utu na heshima zile zile kuhakikisha maisha bora ya vizuka na mayatima ambao hatima yao inatokana na unmwagaji damu wa magaidi hao."

Sudkurier linatukumbusha kwamba ni mwaka mmmoja nyuma pale kizuka wa marehemu Martin Schleyer Bibi gertrude, alipopinga kata-kata kuachwa huru kwa wauaji wa mumewe.

"Wakati ule lilikuwa swali la kutoa msamaha kwa Christian Klar.

Rais Horst kohler alikuwa na haki kukataa kutoa msamaha huo kwa mtu ambae hakuwa hjata tayari kulidhukuru neno "nasikitika" kwa kilichotokea.Mwaka mmoja baadae, swali sio tena kuhurumiwa mfungwa huyo na kupewa msamaha .Mara hii ni sheria ya Ujerumani inayoamua kumtoa gerezani.Kuna wakati inahitaji uvumilivu kuridhiana na sheria kama hizo."

Gazeti la Westdeutsche Zeitung kutoka Dusseldorf likiendeleza mada hii ya Christian Klar laandika:

"Hata ikiwa magaidi wa jeshi Jekundu ( RAF) wakijiita ni wakombozi,walikuwa ni wahalifu na wauaji.Wao wakati ule kama ilivyo sasa, walipaswa kuheshimu sheria...."

Likitukamilishia mada hii kwa leo, Neue Osnabrucker Zeitung laandika:

" Kwa hukumu hii ya kumuacha huru Klar, dola linalofuata sheria linaonesha mamlaka yake.Linaonesha haliongozwi na hisia na kwa kila hali sio dola la kijambazi ambalo Christian Klar aliliona kuwa hivyo."