1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Seoul na China zaahidi kufanya mazungumzo ya kidiplomasia

26 Mei 2024

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol na Waziri Mkuu wa China Li Qiang wamekubaliana leo kuzindua mazungumzo ya kidiplomasia na usalama na pia kuanza tena mazungumzo juu ya makubaliano ya biashara huria.

https://p.dw.com/p/4gIU7
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 3 wa demokrasia mjini Seoul
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 3 wa demokrasia mjini SeoulPicha: KIM MIN-HEE/Reuters

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol na Waziri Mkuu wa China Li Qiang wamekubaliana leo kuzindua mazungumzo ya kidiplomasia na usalama na pia kuanza tena mazungumzo juu ya makubaliano ya biashara huria.

Yoon amemwambia Waziri Mkuu wa China kwamba nchi hizo mbili zinapaswa kufanya kazi pamoja sio tu katika kukuza maslahi ya pamoja bali pia kukabiliana na changamoto za kikanda akitolea mfano wa mzozo wa Urusi na Ukraine na Israel na kundi la wanamgambo la Hamas.

Soma pia: Japan, Korea Kusini zatangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi

Viongozi hao wawili wamekutana siku moja kabla ya mkutano wao na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, mazungumzo ya kwanza ya pande tatu ya majirani hao wa Asia kuwahi kufanyika katika muda wa zaidi ya miaka minne.

China na washirika wa Marekani, Korea Kusini na Japan, zinajaribu kupunguza kuongezeka kwa msuguano kati yao katikati ya ushindani kati ya Beijing na Washington na pia kuhusu mvutano juu ya Taiwan.

Maafisa wanasema matarajio ni madogo kuelekea mkutano huo wa pande tatu japo salamu za kheri kati ya viongozi hao huenda zikasaidia kuchora taswira ya kuwepo kwa uhusiano wa kidiplomasia baada ya miaka mingi ya mivutano.