1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kaskazini na Marekani zaanza luteka ya majini

23 Machi 2023

Vikosi vya Korea Kusini na Marekani vimezindua mazoezi makubwa ya pamoja ya kijeshi yenye kuhusisha meli ya kivita ya Marekani aina ya amphibious.

https://p.dw.com/p/4P70H
Nordkorea Raketentest Miloitärmanöver USA und Südkorea
Picha: Louis Thompson Staats IV/U.S. Navy/ABACAPRESS/picture alliance

Mazoezi hayo yanafanyika siku moja baada ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu.

Jeshi la Korea Kusini limesema takriban wanajeshi 12,000 kutoka nchi hizo mbili watashiriki katika mazoezi hayo, aidha kutakuwa na meli za kivita 30, ndege 70 na magari 50 ya kivita.

Masaa machache baada meli ya kivita kutia nanga, Korea Kaskazini ilifyatua makombora manne kutoka katika pwani yake ya mashariki. Korea Kusini ilisema hatua hiyo inaonesha wazi upinzani wa mazoezi yake na Marekani.